Malezi Daima Foundation watembelea wizara ya Maliasili na Utalii kujifunza ufugaji wa nyuki


Na Mwandishi Wetu,

Wanakikundi wa Chama cha wasanii akinamama Nchini Tanzania kinachofahamika kama Malezi Daima Foundation wametembelea Ofisi za wizara ya Maliasili na Utalii na kujifunza kuhusu ufugaji wa Nyuki.

akizungumzia namna tukio hilo lilivyokwenda, Susan Lewis Natasha amesema kuwa tukio hilo lilikuwa na dhima ya kujifunza kuhusu ujasiriamali wa namna gani asali nyuki wanavyoweza kutengeneza asali, na kujipatia kipato kwa njia sahii na salama.
Baadhi ya Wajumbe wakisikiliza kwa makini

"nimefurahi sana kuhudhuria mafunzo haya kwani nimepata mengi ya kujifunza kuhusu Nyuki na Asali, na ni maeneo gani zaidi yanafaa, na kadhalika. inahitaji umakini na kujipanga vizuri, ambapo vyote vinawezekana ukiwa na nia thabiti ya kujiendeleza" aliongezea Mama Natasha Humba.
Ziara hiyo iliyofanyika juma lililopita ililenga kutoa mwamko kwa kikundi chao na akina mama wengine nchini kwa ujumla, hasa wale wenye nia ya dhati ya kujiendeleza wenyewe kimaendeleo.

Malezi Daima Foundation wakiendelea na mafunzo kwa Teknolojia ya Filamu (Video) wakitazama namna shaghuli nzima zinavyoenda

"kwa upande wangu sioni kama ni dhambi kujiendeleza kiuchumi kwa mwanamke wa leo, kwani ukiwa na akili nzuri ya kijasiriamali, unaweza kuwa imara pasipo kungojea kuolewa, ama kuwaza kuja Jijini Dar es salaam, wakati maeneo hayohayo ya porini yanaweza kukupa utajiri" aliongezea mjumbe mmoja wa kikundi hicho.
Aidha, wanakikundi hao hawakusita kuushukuru uongozi mzima wa wizara akiwemo Afisa wa Wizara hiyo kwa upande wa Misitu, anayefahamika kwa jina la Mama Mapolo kuwa amewaonesha uimara wa mwanamke katika kujiwezesha mwenyewe, na kuahidi kuifanyia kazi elimu hiyo waliyoipata wizarani hapo.

Wanakikundi wa Chama cha Malezi Daima Foundation pamoja na Mtaalamu wa Masuala ya Misitu na Nyuki. Maelekezo hayo yalifanyika kwenye ofisi za Wizara ya Maliasili na Utalii, Mpingo House, Keko Darajani, jijini Dar es salam

Tags: MDF, MALEZI DAIMA, MALIASILI NA UTALII, WIZARA, NYUKI, ASALI

Chapisha Maoni

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Mpya zaidi Nzee zaidi