zile Tuzo maarufu zaidi za filamu zinazotegewa kutazamwa na wengi duniani na 'kususiwa' na mastaa wengi zaidi weusi hasa wa kimarekani, maarufu kama tuzo za Oscars zimedokezwa kuwa na mvuto wa kisasa na wakipekee zaidi kwa watazamaji wake wa mwaka huu.
tuzo hizo zenye kupendelea usiri zaidi katika maandalizi mpaka siku chache kabla ya kuoneshwa, zimedokezwa kuwa zitapambwa na kurembwa zaidi kiteknolojia ya kisasa na mvuto wake utakuwa ni wa kipekee.
akisisitiza ubora huo, Msimamizi wa uandaaji wa sherehe hizo, Derek McLane amedokeza kiduchu kuwa tuzo hizo za mwaka huu zitakuwa na kitu cha kipekee tofauti na miaka mingine yote akishirikiana na Waandaaji wapya (Maprodyuza) David Hill na Reginald Hudlin kazini.
“Nadhani Sherehe zitabeba uhalisia wa Kisasa zaidi” McLane alimjibu mwandishi wa habari nchini marekani. “Kuna matumizi makubwa ya Teknolojia ya LED. Pia kuna matumizi mengi zaidi ya vipande vya video” (Video Footages)
McLane ameongoza (direct) uandaaji wa Tuzo hizo kwa miaka minne mfululizo, na kujishindia tuzo mbalimbali za Emmy na Art director's Guild award kwa kuongoza kuandaa Tuzo za Oscars za mwaka 2014, na ADG ya mwaka 2015 kwa tuzo hizohizo za oscar, zote zikiandaliwa na Craig
Zadan na Neil Meron.McLane amesisitiza kuwa tuzo za mwaka huu zitajitahidi kuelezea namna gani filamu zinavyotengenezwa na kuandaliwa, ambapo tuliona hivyo kwenye tuzo za mwaka 2009 zilizoandaliwa na Bill Condon na Laurence Mark zikishabikiwa kuwa sherehe zenye ubora zaidi za oscar kuliko zote za miaka ya hivi karibuni.
mwaka huo, tuzo zilikuwa zikitambulishwa kirahisi na kwa ufupi kwa mpangilio maalum Kwa mfano: wa mwandishi, na kisha Cinematography na Wahariri baadae. na alipoulizwa kama tutarajie kitu kama hiko tena? akaishia kusema "Labda"
