Katibu Mkuu CHAMUDATA aibuka na Tuzo mbili Africa Shinning Star Awards

Na Mwandishi wetu 

Katibu Mkuu wa Chama cha Muziki wa Dansi Tanzania (CHAMUDATA) ameibuka na tuzo mbili katika Africa Shinning Star Africa Awards, zilizofanyika usiku wa kuamkia tar 8 jijini Kigali, Rwanda.

Akizungumzia ushindi huo, @anania Junior amesema mafanikio hayo si yake binafsi pekee bali ni ushindi wa Tanzania na Watanzania wote, huku akiwapongeza pia Watanzania wengine waliopata tuzo katika hafla hiyo ya kimataifa.

Ushindi huo unakuja ikiwa ni takribani miezi nane tangu achaguliwe kuwa Katibu Mkuu wa CHAMUDATA, hatua inayomfanya pia kuandika historia ya kuwa Katibu Mkuu mwenye umri mdogo zaidi kushika nafasi hiyo tangu kuanzishwa kwa chama hicho zaidi ya miaka 45 iliyopita.

Amesema moja ya ndoto zake kubwa katika uongozi wake ni kuhakikisha muziki wa dansi wa Tanzania unarejea katika ubora wake na kufikia masoko ya kimataifa.

Kwa mujibu wake, licha ya changamoto zinazoikabili tasnia ya muziki wa dansi, anaamini kuwa kwa ushirikiano kati ya viongozi wa CHAMUDATA, wasanii pamoja na Serikali, inawezekana kuurejesha muziki huo katika hadhi na thamani yake.

Aidha, amesisitiza kuwa mafanikio katika tasnia hayawezi kupatikana kwa haraka, bali yanahitaji mipango, mikakati madhubuti na ushirikiano wa wadau wote ili kufikia maendeleo ya kudumu.

Mwisho, alitoa shukrani kwa marafiki, ndugu na wadau wote waliomuunga mkono katika safari yake ya uongozi na maendeleo ya tasnia ya muziki wa dansi nchini.

Chapisha Maoni

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Mpya zaidi Nzee zaidi