Tuzo ya Afrika yamfikia rasmi mhe. Mchengerwa baada ya ushindi, Kigali

Na Mwandishi wetu

Waziri wa Afya, Mhe. Mohamed Mchengerwa, amepokea rasmi tuzo yake ya Shining Star Africa Awards 2026, baada ya kutunukiwa jijini Kigali, Rwanda mapema mwezi huu.

Tuzo ilipokelewa na mshindi ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Muziki wa Dansi Tanzania (CHAMUDATA), @anania.junior na baadae kuikabidhi kwa mhusika. 

Tuzo hiyo inachukuliwa kuwa ni sehemu ya ishara ya kutambua mchango wake katika uongozi na utumishi wa umma barani Afrika.

Mhe. Mchengerwa alishinda katika kipengele cha Best Star Member of Parliament of the Year Africa 2026, tuzo inayotolewa kwa viongozi wanaoonesha utendaji bora na mchango mkubwa kwa jamii katika sekta mbalimbali.


Ushindi huo umeiweka Tanzania kwenye ramani ya viongozi wanaofanya vizuri barani Afrika, huku ukiendelea kuonesha mchango wa viongozi wa nchi katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Tuzo za Shining Star Africa Awards hufanyika kila mwaka nchini Rwanda, zikilenga kuwapongeza viongozi na wanasiasa wanaofanya vizuri katika sekta mbalimbali barani Afrika, na kuhamasisha utawala bora pamoja na maendeleo endelevu.

Kwa wadau wa burudani na tasnia ya sanaa, ushindi huo pia unaonesha jinsi majukwaa ya Afrika yanavyozidi kuunganisha sekta tofauti kuanzia uongozi hadi sanaa ili kutambua mafanikio.

Chapisha Maoni

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Mpya zaidi Nzee zaidi