Dkt. Kasiga: Filamu ni uchumi, utamaduni na daraja la Kiswahili


Na Mwandishi wetu 

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Dkt. Gervas Kasiga, amesema sekta ya filamu nchini ina nafasi kubwa ya kuchangia maendeleo ya kiuchumi, kukuza utamaduni na kuifanya lugha ya Kiswahili kuendelea kusikika katika majukwaa ya kimataifa.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na vyombo vya habari vya serikali, Dkt. Kasiga alizungumzia safari yake kutoka kwenye uandishi wa miswada ya filamu, uigizaji katika kazi mbalimbali za sanaa tangu akiwa Kaole na marehemu Steven Kanumba, hadi kufikia nafasi ya kuiongoza taasisi inayosimamia maendeleo ya tasnia ya filamu nchini.

Kwa mujibu wake, ukuaji wa majukwaa ya kidigitali umefungua milango mipya kwa watayarishaji wa maudhui na kuongeza fursa za filamu za Kitanzania kufikia hadhira ya kimataifa.

Mbali na filamu, Dkt. Kasiga alipongeza mchango wa wabunifu wa maudhui ya kidigitali, wasanii wa stand-up comedy na vijana wanaotumia mitandao ya kijamii kuwasilisha simulizi zinazogusa maisha ya Watanzania.

Alisema ubunifu huo unaonyesha namna sekta ya sanaa ilivyopanuka na kuendelea kubadilika sambamba na maendeleo ya teknolojia.

Dkt. Kasiga pia alimpongeza muigizaji Salim Ahmedy kwa mafanikio ya filamu ya Mwamwindi, akisema kazi hiyo imeonyesha uwezo wa simulizi za Kitanzania kugusa hisia za watazamaji wa ndani na nje ya nchi.

mpaka sasa filamu  hiyo inaendelea kujizolea watazamaji wengi zaidi ikioneshwa YouTube kwenye chaneli yake mwenyewe ya Gabo Zigamba ikijizolea watazamaji zaidi ya 700k ndani ya wiki mbili tuu.

Bodi ya Filamu itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kuboresha mazingira ya uzalishaji wa filamu, kuvutia uwekezaji na kuhakikisha Tanzania inanufaika zaidi na uchumi wa ubunifu unaokua kwa kasi duniani.

Chapisha Maoni

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Mpya zaidi Nzee zaidi