Dkt. Kasiga amkabidhi Stella Mbuge bendera ya Taifa, kuing’arisha Tanzania tuzo za MVAA

Na Mwandishi wetu

Mwigizaji nyota nchini Tanzania, Stella Mbuge (@officialstellambuge) ambaye amechaguliwa kuwania Tuzo za Music Video Africa Awards (MVAA) 2025 katika kipengele cha mwigizaji chipukizi wa kike wa mwaka (Best Upcoming Actress of the Year)

Stella ammbaye ameingia kwenye tuzo hizo kwa kugusa mioyo ya wapenzi wa filamu barani Afrika kupitia tamthilia zake mbili kali za “Nuru” na “Jiya.”

Tuzo hizo zinatarajiwa kufanyika Oktoba 11, 2025, jijini Lagos, Nigeria, zikihusisha pia wasanii wengine kutoka Afrika Mashariki. 

Kabla ya safari yake, Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Dkt. Gervas Kasiga (PhD), alimualika Stella kwenye ofisi za bodi, kule Kivukoni, Jijini Dar es salaam na kumpongeza kwa hatua kubwa ya mafanikio. 

“Tunajivunia mafanikio ya Stella, ni mfano wa juhudi, kipaji na ubunifu wa wasanii wetu,” alisema Dkt. Kasiga.

Zaidi ya hapo, Msanii huyo alimkabidhi bendera ya Taifa la Tanzania kama ishara ya heshima na uwakilishi wa Tanzania kwenye tuzo hizo kubwa za kimataifa, kwa kuiwakilisha vyema

Bodi ya Filamu Tanzania imeahidi kumpa Stella sapoti zote anazohitaji, huku ikiwataka Watanzania wote kumuombea ushindi ili alete heshima kwa taifa letu kupitia filamu. 

Chapisha Maoni

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Mpya zaidi Nzee zaidi