Na Mwandishi wetu
Bodi ya Filamu Tanzania imekutana na viongozi wa Shirikisho la Filamu Tanzania katika kikao maalum kilicholenga kuimarisha ushirikiano na kuboresha utendaji ndani ya tasnia ya filamu nchini.
Kikao hicho kimeongozwa na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Dkt. Gervas Kasiga, na kufanyika leo Ijumaa, Machi 6, 2026, kikihusisha viongozi wa juu wa Shirikisho pamoja na wadau wengine wa sekta hiyo.
Mbali na kujadili masuala ya kiutendaji, kikao hicho kililenga pia kuimarisha mahusiano ya kikazi kati ya taasisi hizo mbili ambazo ni mhimili muhimu katika maendeleo ya tasnia ya filamu Tanzania.
Miongoni mwa waliohudhuria kikao hicho ni pamoja na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Filamu, Emmanuel Ndumukwa, Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Rajab Amir, pamoja na wenyeviti wa vyama tisa vinavyounda Shirikisho hilo
Kwa wadau wa tasnia ya filamu, mikutano ya aina hii ni hatua ya mafanikio ya filamu kwani maamuzi muhimu hufanyika mezani kabla hadithi hazijafika kwenye skrini.