AICFF yapokea kazi za filamu za dini kwa Tamasha la Filamu za Kikristo Afrika 2026



Na Mwandishi wetu

Africa International Christian Film Festival (AICFF) imetangazwa rasmi tuzo za filamu za dini na, au imani ya kikristo, na itafanyika kuanzia Juni 3 hadi 6, 2026 jijini Abuja, Nigeria.

Tamasha hili linakuja kama jukwaa kuu la kuonesha filamu za Kikristo (Kingdom films) kutoka Afrika na duniani kote, sambamba na warsha, mijadala, masterclasses, na soko la filamu za Kikristo. 

Kwa waandaaji wake, AICFF imekuwa kama sehemu ya harakati za kuibua kizazi kipya cha wasimulizi wa hadithi wanaotumia filamu kueneza tumaini, mabadiliko, na maadili, huku wakifungua milango ya Afrika kwa uzalishaji wa filamu za Kikristo za kimataifa.

Watazamaji watapata nafasi ya kushuhudia uchaguzi maalum wa filamu kuanzia filamu ndefu, makala, filamu fupi, na hadi animations; zote zikiwa na ladha ya imani, matumaini na mabadiliko ya maisha.


Aidha, majina makubwa nchini humo, akiwemo Damilola Mike Bamiloye, Fejosbaba, Winlos  na wengine, (ingawa hawajathibitisha), huenda wakawepo kushiriki mijadala hiyo.

Kwa upande wa filamu, manguli mbalimbali wataongoza mijadala kuhusu uandishi wa hadithi, ufadhili, uzalishaji bora, usambazaji wa filamu, na jinsi sinema inaweza kubeba maono ya Ufalme wa Mungu bila kusahau namna ya kuwafikia watazamaji wengi zaidi.

Mpaka sasa, Nigeria imekuwa kinara wa kuzalisha filamu za imani ya kikristo kwa wingi, maarufu kama filamu za dini (Christian faith based films) ambazo zimejipatia umaarufu mkubwa sana barani afrika na kwingineko duniani kote kwa muundo wake wa asili.

Kushindana huko kunalenga kuimarisha maadili ya kiafrika ambayo yanashabihiana na jamii zote barani Afrika kusini mwa jangwa la sahara ikiwemo nchi za ukanda wa afrika mashariki

Kwa upande wa mafunzo, AICFF itatoa programu za kujenga uwezo kwa watengeneza filamu wa Afrika katika nyanja mbalimbali ikiwemo uongozaji, uandishi wa miswada, upigaji picha, sauti, uhariri, na biashara ya filamu, kwa lengo la kuwapeleka kutoka wazo hadi kuonekana kwa uthabiti.

Soko la filamu za Kikristo limejipatia umaarufu mkubwa barani Afrika huku Nigeria wakiwa vinara katika kuzalisha filamu hizo, na sasa zina wataalamu wengi mbalimbali maarufu wanaolipwa fedha nyingi kwa uigizaji, na kupata casts hadi nchi za ulaya na Amerika.


Tamasha hilo pia litatunuku tuzo kwa mafanikio bora katika sinema ya Kikristo, zikiwemo tuzo za Best Screenplay, Best Cinematography, Best Director, Best Actor/Actress na nyinginezo, hatua itakayowapa heshima wasanii na wabunifu waliobeba ujumbe wa imani kwa ubora wa hali ya juu.

Maombi ya kushiriki filamu tayari yamefunguliwa kupitia FilmFreeway, na moja kwa moja kwenye site yao, huku mwisho wa kutuma kazi ukiwa ni Machi 31, 2026, kabla ya tamasha kufanyika Juni mwaka huo. 

Watakaopata nafasi ya kushiriki watakuwa sehemu ya harakati mpya za kuiweka Afrika katikati ya ramani ya sinema ya imani duniani.



Chapisha Maoni

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Mpya zaidi Nzee zaidi