MIMI NA ANGOLA ni historia ya kweli ya maisha ya
mwanaswahiliwood susan natasha humba zamani alijulikana kama susan lewis
natasha.
Fuatilia kisa hiki cha kusisimua……
…..ilikuwa ni miezi michache imepita toka
nilipofanya kosa kubwa sana lililobadilisha maisha yangu yote. kosa ambalo si
tu lilinifanya kujuta na kujiona kama sina thamani tena maishani, lakini pia ni kosa lililonitoa
eneo moja na kunipeleka eneo jingine.
Sikuweza kujitoa kwa vile maji yakimwagika hayazoleki kwa hiyo ilibidi niwe
mpole na kukubali matokeo.
Siku isiyo na jina, baba yangu mzee Ngatwika
alirudi nyumbani toka kazini akionyesha furaha na kuwa ana neno la kusema, mimi
na mama ilibidi tukae kimya kumsikiliza baada ya kupata chakula cha jioni .
“nimepata uhamisho wa kwenda Angola, natakiwa
niwe nimeripoti ubalozini ndani ya miezi miwili toka sasa”
Wote tulillipuka kwa furaha na baada ya sekunde
kadhaa wote tulibaki kimya huku kila mmoja akizama kwenye mawazo yake binafsi.
Sijui mama na baba walikuwa wakiwaza nini ila
kwa upande wangu nilijiona kuwa nina bahati mbaya maana kama nilivyosema hapo
awali ilikuwa ni miezi michache toka nimetenda kosa kubwa maishani na kosa
lenyewe linaweza kunifanya nisiende hii safari tofauti na safari zote
wanazokwenda wazazi wangu,
ni kosa gani hilo
alilofanya Susan linalomyima raha? Huo ni mwanzo tu wa tamthilia hii tamu ya
simulizi, endelea kufuatilia ujue