Kama umebahatika kuona tamthilia ya THE TEAM utakubaliana nami pia namna kazi za Director huyu mwanadada anayepata umaarufu wake katika kazi za filamu kwa kasi, ila utakapobahatika kuitazama au kuiangalia filamu ya HOMECOMING utaelewa ni jinsi gani alivyoamua kwenda next level.
Hapa nitaongelea yaliyotokea behind the scene nikiwa kama mmoja wa waigizaji niliyeigiza kwa jina la auntie Rehema, mke wa waziri mstaafu mhe. Mshindi (hashim kambi) ingawa jina langu halisi ni Susan natasha Humba.
ENjoy!
![]() |
|
Nimecheza kama Auntie Rehema, Mke wa waziri mstaafu Mh. Mshindi, na pia
mlezi wa abel (Daniel kijo) aliekuwa kinara wa filamu ya homecoming.
|
![]() |
| Starring of the Film, Daniel Kijo. Mtangazaji wa Awali wa vipindi vya Televisheni, 5 Connect (EATV) na Daladala |
Directors walikuwa wawili, mmoja toka Africa kusini na mwingine ni mwanadada Seko Shamte akiwa ni director mkuu. Mpiga Picha D.O.P (director of photograph) alikuwa mmarekani na msaidizi wake wakiwa wanatumia mojawapo ya kamera bora za wakati huu.
![]() |
Tulifika pale saa 12 asb na kutoka saa 7 mchana.
BAADA ya hapo goma liliendelea kwa siku 20 mpaka kumalizika shooting nzima.
Nakumbuka
scene nyingine niliyoshiriki iliyochukua muda mrefu ni ya sherehe ya
kumkaribisha abel aliekuwa amerejea nyumbani tz toka marekani masomoni. ![]() |
| HAPA dada wa makeup alikuwa kazini…… |
Waswahili wanasema "shida haikosekani kazini" hata siku ya harusi katika bahati mbaya sana kuna kosa lilifanyika ambalo halikuweza kuzuilika, kwani nguo niliyoivaa airport niliondoka nayo sikuiacha kama zile zingine na niliporudi siku nyingine kwa ajili ya scene ya sherehe, ikawa haipo ingawa ilitakiwa. Ikabidi director afanye marekebisho ya chap chap. Pole sana Seko.
![]() |
|
Airport
nilipompokea Abel nilionekana hivi…..
|
![]() |
|
Na
kwenye sherehe ingawa ilikuwa ni siku hiyohiyo (kama inavyosema script) nilikuwa na muonekano huu….
|
Ni
kosa kubwa sana kwa mwigizaji kuondoka na nguo ya shooting, lakini waswahili wanasema ajali kazini!
![]() |
| Susan Natasha Humba, Mama Abdul na Mama Shela |
Shooting
iliendelea na waigizaji waalikwa walikuja katika scene hiyo ya sherehe…
Pamoja
na waigizaji wengine waliokuwepo mzee chilo alikuwa ni mchumba wangu utotoni
(kwenye filamu)
![]() |
| Baba wa Abel katika pozi |
scene hii tuliipigia mabwepande na ilikuwa mara yangu ya kwanza kufika eneo hilo. Na ujanja wangu woote ila sijawahi kufika eneo hili. (kumbe jiji la Dar ni kubwa namna hii?).
![]() |
| Mapumziko kazini |
Kuonyesha
wako vizuri kila idara tulikula vizuri
na kunywa.
kuanzia chai saa 12 asb, chakula cha mchana
muda muafaka na vitamtam vya kumwaga
na after lunch tulipumzika kama
hivi.
Huyo
mkaka mbele ndie director toka South Africa na huyu mzungu nyuma ni msaidizi wa mpiga
picha , nilipewa story yake na d.o.p alifanyaga kituko flani amazing huko kwao,
nilicheka sana na kuanzia siku hiyo nilimpachika jina la 'Mr. Trouble-some'.
Kwa
upande wangu nimefurahi kufanya kazi na cast na crew wote wa filamu ya homecoming bila kumsahau muddy niliyekuwa nikimwamsha
saa 10 na nusu usiku kwa ajili ya kwenda shooting kisa eti nampitia!
![]() |
| Katika filamu kuna scene mbalimbali za mahela na haya ndio yaliyotumika |
Pia nakupa big up nyingi saaaana sana sanaaaa director Seko Shamte ukiungana na madirector wanawake wenzako, Honeymoon Aljabri wa filamu ya Daddy's Wedding, Leah Mwendamseke alieongoza filamu kadhaa za bongo muvi na
Yvonne Cherrly (Monalisa) ambaye pia ameongoza filamu kadhaa ikiwemo chanzo ni mama.
Niliyekuandalia kitu hiki kizuri, Ni mimi mwanaswahiliwood, Sinyora Susan Natasha Humba (kubwa la maadui)

















