Uzinduzi wa filamu ya Homecoming (2015) umeandika historia mpya na ya kipekee baada ya kupongezwa na wadau mbalimbali waliojitokeza kuitazama kwa mara ya kwanza kwenye ukumbi wa Filamu wa Century Cinemax, Mlimani City Mall, Jijini Dar es salaam
wakati akifungua rasmi utazamaji wa filamu hiyo kwa mara ya kwanza (Screening), Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Mh. Nape Nnauye amependezwa na maendeleo ya filamu za Kitanzania kwa kuzingatia maadili, utamaduni na kukuza lugha ya kiswahili, kwani ni hatua kubwa zaidi katika ukuaji wa sekta ya filamu.
“Nimefarijika sana kuona leo tumekusanyika kwenye ukumbi huu kwa ajili ya kuzindua filamu ya Kitanzania, hivyo niwapongeze wamiliki wa ukumbi huu kwa kuruhusu kuonyeshwa kwa filamu hii hapa, najua ni mwanzo na itakuwa faraja zaidi siku nyingine nikija hapa nikute filamu zetu zikionyeshwa maana najua huwa ni adimu mno kuona sehemu kama hii watu wameketi kuangalia filamu zetu..
kwa upande mwingine, katibu mtendaji wa bodi ya filamu nchini, Joyce Fisoo ameipongeza hatua ya kipekee kufanikiwa kuoneshwa kwa mara ya kwanza kwenye ukumbi wa filamu wa Century Cinemax, na kuongezea kuwa inawezekana, kama filamu ikivuka vigezo elekezi vya ubora unaohitajika
"kuoneshwa kwenye Jumba la sinema ni hatua kubwa sana na ya kipekee, hatuna budi kujivunia, kwa kweli, ingawa haikuwa kazi rahisi." aliongezea mama Fisoo
mmoja wa waigizaji wa filamu hiyo, Susan Lewis Natasha aliizungumzia filamu hiyo kuwa imefanikiwa kuuleta ubora halisi wa filamu ya Tanzania. "Najisikia furaha sana kuona filamu ya kitanzania ikioneshwa Cinema kwa screening ya kipekee. hii inaonesha ni namna gani tunakubali maendeleo kwa kuyasogelea mbele kule yalipo" aliongezea Susan.
![]() |
| Director/ Producer wa filamu ya Homecoming, Seko Shamte |
Filamu hiyo imekutanisha mastaa wengi wa Filamu nchini Tanzania, na wengineo kutoka barani Afrika akiwemo Staa aliyeshiriki Big Brother Africa ya mwaka 2003, Abby Plaatjes.
Baadhi ya mastaa hao walioshiriki katika filamu hiyo ni pamoja na aliyekuwa akitangaza kipindi cha 5 Connect na baadae, Daladala Daniel Kijo ambaye ndiye Muigizaji mkuu wa filamu hiyo. Waigizaji wengine ni pamoja na Ahmed Olotu ‘Mzee Chilo’, Hashim Kambi, Susan Lewis ‘Natasha’
Waigizaji wengine walioigiza katika filamu hiyo ni Alpha Mbwana, Magdalena Munisi, Godliver Gordian na Michael Kauffmann.
Filamu hiyo inatarajiwa kuanza kuoneshwa rasmi kwenye Kumbi mbalimbali za Cinemax nchini kuanzia Januari ya Tar. 29 mwaka huu.
kwa maelezo zaidi, na kutazama trailer la filamu hii, tembelea http://www.homecomingtz.com/homecomingtrailer/




