
Naibu waziri wa habari, utamaduni sanaa na michezo, Mh. Anastazia Warioba atembelea kijiji Cha wasanii kilichopo Mwanzenga, wilaya ya Mkuranga na kujionea mwenyewe maendeleo ya Kijiji hicho cha wasanii Mkoa wa Pwani.
Akiongozana na Mkuu wa wilaya ya mkuranga, Mh. Anastazia amefurahishwa na maendeleo ya kijiji hicho licha ya kuwepo kwa changamoto kemkem zinazowakabili wasanii hao ambazo ameahidi kuzitafutia ufumbuzi kwenye ngazi husika.
Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Mkuranga, Mh. Abdallah Ali Kihato amesisitiza kuwa changamoto kuu zinazokikabili kijiji hicho zinaendelea kushughulikiwa ambapo tarari umeme upo karibu sana kuingia kijijini hapo, na Miundombinu ya barabara bado inafanyiwa kazi.
aidha, wasanii walifurahishwa sana kutembelewa na Mh. Naibu waziri, na kuongeza kuwa amewatia moyo wa kipekee kwa namna ya utendaji wa serikali ya Awamu ya Tano katika muendelezo wa maendeleo ya sanaa nchini kama ilivyoazishwa na serikali zilizopita na kumuomba aendelee kupigania maendeleo ya wasanii hadi kufikia panapostahili, ili kuiendeleza pia jamii yetu.
tukio hilo lilihudhuriwa na Mgeni Rasmi, Naibu waziri wa habari, utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Annastazia Wambura pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Mtandao wa wasanii Tanzania (SHIWATA) pamoja na wasanii mbalimbali akiwemo Ahmed Ulotu (Mzee chilo), Susan Lewis (Natasha) na wengineo.



