Msiba wa Edwin Semzaba ni Pigo kwa Wanafasihi ya Kiswahili Ulimwenguni.

Mwandishi wa vitabu vya Kiswahili kikiwemo, Ngoswe: Penzi Kitovu cha Uzembe, Edwin Semzaba amefariki dunia Jumapili ya January, 17 mwaka huu.

Akiwa mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, UDSM kwenye idara ya sanaa za maonesho, alifundisha masomo ya Uandishi wa Ubunifu/Miswada ( Creative Writing/Script) na kuigiza (acting). Semzaba anakumbukwa kwa uandishi wake mahiri hususan kwa kitabu cha mchezo wa Ngoswe; Penzi Kitovu cha Uzembe kilichotumika kwenye shule za sekondari katika somo la Kiswahili.

ameishi katika sanaa kwa muda mrefu sana, akiwa mwanafunzi wa miaka 16 aliweza kuandika tamthilia ya Ngoswe kama mchezo wa kuigiza, ambapo baada ya kupata umaarufu nchini kupitia Redio Tanzania Dar es salaam (RTD) ndipo kikachapishwa na kumpa Umaarufu zaidi Nchini na kwa wapenda Fasihi ya kiswahili ulimwenguni kote, ambapo mpaka leo hii kitabu hicho kinatumika kufundishia kwenye Mtaala wa kiswahili kama Tamthilia, kwa upande wa Fasihi Andishi.

pia Marehemu Semzaba amekuwa msanii kwa kucheza baadhi ya maigizo katika taaluma yake, na pia kuandika na/au kuongoza baadhi ya michezo ya jukwaani.
 Michezo aliyoiandika ni pamoja na Kinyamkera (2014), Joseph na Josephine (2014),
Baadhi ya vitabu vya hadithi alivyoandika ni pamoja na Tendehogo (1982), Sofia wa Gongo la Mboto (1985) Mkokoteni (1988), Tausi wa Alfajiri (1996), Funke Bugebuge, (1999),  na Tamaa ya Boimanda (2002) Marimba ya Majaliwa (2008)

ameshinda Tunzo yake ya kwanza ya Waandishi wa Afrika ya Mashariki kutoka Taasisi ya Uchunguzi (Utafiti) wa Kiswahili (TUKI) kwa riwaya yake ya Funke Bugebuge; na baadae, "grandchildren's adventure book writing competition" aliyotunukiwa na Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania (2007).

Bibliography

Riwaya

  • Marimba ya Majaliwa, E & D Vision Publishing, 2008
  • Funke Bugebuge, Dar es Salaam University Press, 1999.
  • Tausi wa Alfajiri, HEKO Publishers, 1996
  • Tamaa ya Boimandaa Dar es Salaam University Press,2002

Tamthilia

  • Kinyamkera, Exodia Publishers, 2014.
  • Joseph na Josephine, Exodia Publishers, 2014.
  • Ngoswe, Dar es Salaam University Press, 1996.
  • MkokoteniExodia Publishers,2014
  • Tendehogo Tanzania Publishing House (TPH), 1982
  • Sofia wa Gongolambotoa Benedictine Publications, Ndanda,1985.

  Tuzo na Tunuku (heshima)

  • First Prize Winner Western Zone Sabasaba Writing /Reciting Poetry competition at Kigoma 1967.
  • Best Actor Award at Mkwawa High School - 1971-1972
  • First Prize Winner Playwriting Competition Literature Dept (UDSM) 1975
  • First Prize Winner, Novel Writing Competition East African Litrerature Bureau and TUKI(UDSM) 1976.
  • First Prize Winner SIDA Children Adventure Book Competition,2007.
  •  
    Chanzo Wikipedia na Mitandao mingine ya kijamii

Monalisa Tanzania

Hi! karibu katika blogsite yangu ya Monalisatanzania. upate kunifahamu japo kwa ufupi na kipekee kama shabiki au mpenzi wa kazi zangu. utapata habari, burudani na taarifa official kutoka kwangu. enjoy!

Mpya zaidi Nzee zaidi