![]() |
| Mwenyekiti anayemaliza muda wake wa Chama cha Watayarishaji Filamu Tanzania (CHAWAFITA) William Mtitu (PICHA na Global P.) |
Akizungumza na waandishi wa habari, mwenyekiti wa muda wa chama hicho, Mtitu amesema kuwa wanaotaka kuwania uongozi wajitokeze pia na kuwania nafasi mbalimbali. "Kwa wanachama wote watakao kuwa tayari kugombea uongozi wa chama cha Watayarishaji wa Filamu Tanzania (CHAWAFITA), kwa nafasi za uongozi kama ifuatavyo; nafasi ya Mwenyekiti wa chama, M/kiti msaidizi wa chama na wajumbe wa bodi, fomu zitaanza kutolewa kwa wanachama tarehe 1/02/2016 hadi tarehe 10/02/2016, ambayo itakuwa mwisho ili kupisha uchaguzi." aongezea.
Gharama za fomu za kugombea uongozi wa Chama cha Watayarishaji wa
Filamu (CHAWAFITA) zitatofautiana kiwango cha pesa kulingana na ngazi za uongozi kama ifuatavyo
Mwenyekiti wa Chama shilingi 50,000 za kitanzania
M/Kiti msaidizi wa chama shilingi 30,000 za kitanzania
Wajumbe wa Bodi shilingi 20,000 za kitanzania.
Uchaguzi wa Chama cha Watayarishaji wa Filamu Tanzania (CHAWAFTA) unatarajiwa kufanyika tarehe 17/02/2016.
Kwa maelezo zaidi au jinsi ya kupata fomu waandikie kwenye barua pepe ifuatayo; chawafitatz@gmail.com au uwapigie kwenye simu zifuatazo +255767291414/+255654070055/+255684333375/+255653114444
Imetolewa na uongozi
Chanzo: FilamuCentral
