Muigizaji Maarufu duniani Will Smith amejiunga na mkewe Jada Pinkett Smith kusisitiza kutohudhuria sherehe za tuzo za Oscar (Academy awards), zitakazofanyika Februari 28 nchini marekani kugomea mwelekeo hafifu wa washiriki weusi kwenye makundi (categories) muhimu mwaka huu.
Uamuzi huo wa Smith umekuja kutokana na malalamiko ya wengi yanayoendelea kuzidi kwenye Chuo hicho cha sanaa na Sayansi ya Sinema yanayopelekea mwitikio wa wengi wauitao Uelekeo tata wa "Mfumo" huo
akizungumza na kituo kimojawapo cha televisheni asubuhi ya jana, amesema kuwa hajihisi mwenye raha kutokana na hali hiyo. "kwa miaka miwili mfululizo, washiriki wote (20) wa Uigizaji ni weupe.
“Mke wangu haendi, Itakuwa fedheha nikionekana na Charlize (Theron)". "Tumelijadili hili. sis ni sehemu ya hii jamii. lakini kwa wakati huu, tunajihisi vibaya kusimama na kusema, 'Hii ni sawa'
Smith aliwahi kushindania tuzo za Oscar mara mbili, kama muigizaji bora wa kiume, mwaka 2001 na Filamu iitwayo "Ali" na mwaka 2006 na filamu yake iitwayo "The Pursuit of Hapiness". alikosa mara zote mbili mbele ya mastaa wenzie weusi, Denzel Washington's "Training Day" na Forest Whitaker akicheza filamu ya "The Last King of Scotland" (2006).
“kwa upande wangu, huo ulikuwa ni upekee. ila ninapotazama orodha hii na 'Tamthilia' ya washindani waliotangazwa-na kila mmoja yuko safi sana, anatisha, na ndipo mkanganyo unapokuja wa jambo hili.....lakini nahisi kama inaelekea kwenye uelekeo usio sahihi." aliongezea, smith.
Smith alidai kuwa ana jukumu la kusema ukweli au kuhatarisha katika kuchangia tatizo.
“kuna wakati tuna dhamana kubwa kwenye jamii na endapo tusipokuwa sehemu ya suluhu, basi tutakuwa sehemu ya tatizo. na ni yeye pekee (mkewe) aliyeamka na kuitikia kitendo hicho, (wiki iliyopita) kwa upande wake mwenyewe, na kwa upande wangu na kwa familia yetu kuwa sehemu ya suluhisho"
“hii ni muhimu zaidi si kwangu mimi, hapana, bali kwa watoto ambao watakaa chini na kutazama Sherehe hizo, na kutojiona wakiwakilishwa (na mtu yeyote mweusi)....upo udhalimu na ubaguzi wa kidini na ki-rangi ambao unaonekana Holywood, unaoweza kuja kuiathiri hata nchi yetu na si vizuri kuuacha uendelee" alisisitiza smith akiongea na "Good Morning America"
Will Smith, amekosa kuingia kwenye Tuzo hizo za Oscar kutokana na filamu yake mpya ya Concussion kutemwa nje ya washindani hao wa Academy, na kufanikiwa kuingia filamu moja pekee ya "Straight Outta Compton", ambayo ushindani uliopo haujamhusisha mtu yeyote mweusi kwenye uigizaji.
Hasira zimetawala kutoka sehemu mbalimbali kuelekea uteuzi wa washiriki wa tuzo za mwaka huu zinazoendelea kuchemka mpaka hivi sasa. Jada Pinket Smith alitoa hisia zake za moyoni wiki iliyopita mara baada ya kutangazwa kwa washiriki/washindani hapo Januari 14.
Pia, Muongozaji Spike Lee alijiunga naye katika 'mgomo' huo ingawa Jumatano iliyopita Lee aliweka sawa (alipohudhuria kwenye GMA) alipokuwa anaongea na mtangazaji George Stephanopoulos kuwa hawahamasishi wengine kugomea sherehe hizo.
pia, Jumatano hiyohiyo, Mwanachama wa zamani wa bodi ya AMPAS Quincy Jones alisema atajaribu kuifikia bodi ya sasa juma lijalo kuhusiana na tatizo hilo. Jones ndiye Mmarekani mweusi wa kwanza kuteuliwa kwenye Bodi ya chuo ya magavana na mmarekani mweusi wa kwanza kutunukiwa tunzo ya kwanza ya Academy's Prestigious Jean Hersholt Humanitarian Award. Pia ni Mshindani mara nne wa tuzo za oscar (NOMINATED) na alidhamini maonesho ya televisheni (Telecast) ya Oscar mwaka 1996
![]() |
| Filamu Mpya ya Will (2016) |
akizungumza na kituo kimojawapo cha televisheni asubuhi ya jana, amesema kuwa hajihisi mwenye raha kutokana na hali hiyo. "kwa miaka miwili mfululizo, washiriki wote (20) wa Uigizaji ni weupe.
“Mke wangu haendi, Itakuwa fedheha nikionekana na Charlize (Theron)". "Tumelijadili hili. sis ni sehemu ya hii jamii. lakini kwa wakati huu, tunajihisi vibaya kusimama na kusema, 'Hii ni sawa'
Smith aliwahi kushindania tuzo za Oscar mara mbili, kama muigizaji bora wa kiume, mwaka 2001 na Filamu iitwayo "Ali" na mwaka 2006 na filamu yake iitwayo "The Pursuit of Hapiness". alikosa mara zote mbili mbele ya mastaa wenzie weusi, Denzel Washington's "Training Day" na Forest Whitaker akicheza filamu ya "The Last King of Scotland" (2006).
![]() |
| Hapa Will Smith akicheza kama Muhammad Ali katika filamu ya "Ali"(2001) |
“kwa upande wangu, huo ulikuwa ni upekee. ila ninapotazama orodha hii na 'Tamthilia' ya washindani waliotangazwa-na kila mmoja yuko safi sana, anatisha, na ndipo mkanganyo unapokuja wa jambo hili.....lakini nahisi kama inaelekea kwenye uelekeo usio sahihi." aliongezea, smith.
Smith alidai kuwa ana jukumu la kusema ukweli au kuhatarisha katika kuchangia tatizo.
![]() |
| Moja ya Scene za kwenye filamu aliyocheza ya "The Pursuit of Happiness" (2006) |
“kuna wakati tuna dhamana kubwa kwenye jamii na endapo tusipokuwa sehemu ya suluhu, basi tutakuwa sehemu ya tatizo. na ni yeye pekee (mkewe) aliyeamka na kuitikia kitendo hicho, (wiki iliyopita) kwa upande wake mwenyewe, na kwa upande wangu na kwa familia yetu kuwa sehemu ya suluhisho"
“hii ni muhimu zaidi si kwangu mimi, hapana, bali kwa watoto ambao watakaa chini na kutazama Sherehe hizo, na kutojiona wakiwakilishwa (na mtu yeyote mweusi)....upo udhalimu na ubaguzi wa kidini na ki-rangi ambao unaonekana Holywood, unaoweza kuja kuiathiri hata nchi yetu na si vizuri kuuacha uendelee" alisisitiza smith akiongea na "Good Morning America"
![]() |
| Filamu maarufu aliyowahi kuongoza Spike lee |
Hasira zimetawala kutoka sehemu mbalimbali kuelekea uteuzi wa washiriki wa tuzo za mwaka huu zinazoendelea kuchemka mpaka hivi sasa. Jada Pinket Smith alitoa hisia zake za moyoni wiki iliyopita mara baada ya kutangazwa kwa washiriki/washindani hapo Januari 14.
Pia, Muongozaji Spike Lee alijiunga naye katika 'mgomo' huo ingawa Jumatano iliyopita Lee aliweka sawa (alipohudhuria kwenye GMA) alipokuwa anaongea na mtangazaji George Stephanopoulos kuwa hawahamasishi wengine kugomea sherehe hizo.
pia, Jumatano hiyohiyo, Mwanachama wa zamani wa bodi ya AMPAS Quincy Jones alisema atajaribu kuifikia bodi ya sasa juma lijalo kuhusiana na tatizo hilo. Jones ndiye Mmarekani mweusi wa kwanza kuteuliwa kwenye Bodi ya chuo ya magavana na mmarekani mweusi wa kwanza kutunukiwa tunzo ya kwanza ya Academy's Prestigious Jean Hersholt Humanitarian Award. Pia ni Mshindani mara nne wa tuzo za oscar (NOMINATED) na alidhamini maonesho ya televisheni (Telecast) ya Oscar mwaka 1996
![]() |
| Quincy Jones, aliyewahi kufanya vizuri sana kwenye ulimwengu wa filamu duniani |