![]() |
| Wanamichezo wa sarakasi wakifanya yao viwanjani hapo |
Tamasha la Sanaa Utamaduni na Michezo lililoandaliwa na halmashauri ya wilaya ya Mkuranga limefana kipekee Jumamosi ya jana kwa kuwahusisha wasanii mbalimbali waliolipamba vyema tamasha hilo lililofanyika katika ukumbi wa Highway, Mkuranga Mjini, Pwani.
Akiongea kwa upande wa wasanii, Katibu wa SHIWATA amesema kuwa wasanii wa wilayani hapo walijitokeza kwa wingi na kushiriki vyema kwenye tamasha hilo lililopambwa na wasanii nyota na maarufu nchini akiwemo Kulwa Kikumba (Dude), Ahmed Ulotu (Mzee Chilo), Susan Lewis (Natasha) na Msanii wa Muziki aliyejizolea umaarufu wake kwa kuimba na 'kitambaa cheupe' maarufu kama King Kikii
![]() |
| Wasanii Mbalimbali waliohudhuria tamasha hilo |
sherehe hizo zilizotarajiwa kuhudhuriwa na Mkuu wa wilaya ya Mkuranga, ambaye aliwakilishwa na kaimu katibu tawala wa wilaya ya Mkuranga, Clement Muya akiwa mgeni rasmi wa tamasha hilo. wageni wengine waliohudhuria tamasha hilo ni pamoja na Mwenyekiti wa chama cha waigizaji Tanzania (Wilaya ya Kibaha) wasanii maarufu, wawakilishi kutoka BASATA, na wawakilishi wengine kutoka wilayani Mkuranga.
![]() |
| Sarakasi ya baiskeli |
wakati akionesha kufurahia tamasha hilo, msanii Nyota wa filamu nchini, Ahmed Ulotu alijitolea kufanya kazi na msanii yeyote mwenye kazi yake na kuongezea kuwa yuko tayari (yeye pamoja na wenzie waliohudhuria) kusaidia kuicheza filamu hiyo.
"Nimefurahi sana kuwa hapa. wasanii wa wilaya ya mkuranga wameonesha mwamko mkubwa sana kwenye tamasha hili, na nimedhani ni vyema sana tukifanya nao kazi, na kuwasaidia pale inapobidi" aliongezea, Mzee Chilo.
![]() |
| Wananchi waliojitokeza eneo hilo kushuhudia tamasha Hilo Mjini Mkuranga |
Kutazama Picha zaidi, Ingia HAPA



