MIMI NA ANGOLA
SEHEMU
YA TATU
Nakumbuka siku moja tulikuwa tunacheza jioni
maeneo ya kulaza magari mara tukamwona mfanyakazi wa ndani anakuja akiwa na wasiwasi akatukutanishana watoto
wote na kutuamuru twenda eneo Fulani mle mle kwenye eneo letu la
diplomats na kutuweka pamoja kama vile kuna vita, eneo zima lilikuwa limezizima
kwa hofu na sintofahamu. Baada ya dakika
chache tukaruhusiwa kurudi majumbani mwetu na kuambiwa kilichotokea, kumbe
umeme ulikatika kwa dakika 2 tu! Sikuwahi kuona umeme ukikatika miaka yote
mitano tuliyokaa china! Tanesco mpo
hapo?
Hii
ni hadithi ya maisha yangu ikiandikwa na mimi mwenyewe.
Susan
natasha humba.
Endelea
sura ya nne ya mimi na Angola……
Miaka
kadhaa ikapita tumerudi Bongo mwaka 1975 ambapo kukatika umeme ni kitu cha kawaida.na
mbaya kuliko yote tulikuwa katikati ya miezi kumi na nane ya kujifunga mkanda
baada ya vita ya Uganda na Tanzania,ugali wa njano na harage chungu,kila kitu
kwa foleni huku magari ya mobile shop yanayuouza unga na bidhaa muhimu ya
yakikimbiliwa kila yanapopita mtaani watu kuwahi kuweka mawe kwenye foleni.
Ndipo baba alipopata barua ya uhamisho kwenda angola wakati mchele ulikuwa ni bidhaa adimu ukienda sokoni tandika unaona
punje chache za mchele zimewekwa juu ya gunia,unasimama na kutoa pesa huku
ukiwa peke yako bila muuzaji ingawa yuko mahali akikuangalia na kuhakikisha uko
peke yako bila polisi au mpelelezi ndipo muuzaji anakuja fasta anachukua
pesa hamna hata salamu anapotea akirudi anakuja na mchele uwe mzuri
au mbaya,kilo imetimia au la,
utajiju. Tena kwa mtindo huu
tukienda sisi watoto tunapata lakini alikuwa akienda mama yangu wanamnyima kisa
eti wanamshuku.
“uza
uone. Huyu scrurite shauri yako!
(wanadhani mama ni security yaani mpelelezi, ingawa sio kweli kisa eti
muonekano wake na pia anavaa miwani)
Katika
kipindi hiki kigumu ndipo baba anapoleta habari nzuri kama hii.
“nimepata
uhamisho kwenda Angola ……. Hata kama ungekuwa wewe usingefurahi?
Tulikuwa
tumekaa kimya kila mmoja akitafakari kwa upande wake kivyake.
Kwa
upande wangu nilijiuliza maswali mengi mojawapo likiwa je? Ntakwenda?
Maana ni kipindi kifupi nimetoka kufanya kosa kubwa lililobadili mwelekeo wa maisha yangu toka
hali ya utoto niliokuwa nayo hadi utu uzima.
Kifupi
ni kwamba nilitoka kujifungua mtoto mzuri wa kike waswahili wangemwita mwanaharamu, hana
baba na mimi mama yake sina msimamo
wowote wa maisha sikuwa na kazi wala
uwezo wa kumlea.
Baada
ya kumaliza darasa la saba shule ya msingi temeke nilienda shule ya sekondari na ufundi bagamoyo nikasoma kwa miezi michache na kuacha kwa
vile fani nilizozitaka hazikuwepo
nilirudishwa nyumbani nisubiri kwenda shule nyingine na wakati huo wa kusubiri
nikafanya utundu mara ya kwanza maishani
na kupata mimba.
Hapa
nilipo nimempakata mtoto ambae baba yangu alipomwona tu akitoka hospitali
alimpenda na alimpa jina la mpenzi wangu
akawa anampenda kuliko kitu chochote duniani akirudi kazini jambo la kwanza ni
kumbeba na kumrusharusha na kuuliza ameshindaje. Usiku mtoto alikuwa ni mlizi
sana baba huwa anaacha kitanda na kuja kumbembeleza na kunipa ruhusa nikalale
kifupi alitujali kama vile sikuwa nimemfanyia kosa lolote.
Asante
baba sina cha kukulipa.I love you dad!
Kama
vile baba alijua ninachowaza alikata ukimya ule.
“suzy
tutakwenda nae,hatuwezi kumwacha na mtoto mchanga hivi au siyo mama? Pia
tutaenda na Tony”
(Rose
kwa wakati huu alikuwa ameshaolewa na Tony ni mdogo wangu wa mwisho aliezaliwa
china)
Mama
alikubali moja kwa moja na kuanza maandalizi.
Utata ukatokea lilipotakiwa jina la mtoto kwa ajili ya kuwekwa kwenye
passport wote tukawa kimya.baba aliibuka na wazo.
“kwa
vile mimi namwitaga mpenzi wangu basi kwa nini tusimwite hilo hilo jina la
mpenzi ila kwa kifaransa nadhani litafaa na aitwe cherrie.
Likaonekana
ni wazo zuri tukalipitisha jina hilo
akaitwa cherrie ama kwa Kiswahili Sherry.
siku ya kuondoka ilifika nakumbuka siku hiyo
majira ya saa sita ulipikwa ugali wa njano na maharage mekundu chakula ni
kichungu kibaya lakini ndio hivyo lazima ule ili usife,gari lilikuja na tukajipakia
kuelekea uwanja wa ndege saa nane tulitakiwa kuwasili uwanjani.
Baada
ya muda tuliingia ndani ya ndege na kwa kupitia madirisha madogo ya ndege
nilikuwa nikiwaangalia ndugu waliokuja kutuaga uwanjani machozi yalikuwa
yakinitoka kila nikiwaangalia.
Taratibu
ndege ilianza kuondoka huku nikiwaangalia,ilipofika mahali pa kusimama na
kuongeza kasi ya injini nililaza kichwa kwenye kiti huku uso ukiangalia mbele
sikuangalia tena dirishani huku nimempakata sherry wangu ndege ilianza kuondoka
kwa kasi na kuendelea kushika kasi hadi ilipoiacha ardhi na kupaa juu
niliendelea kubaki vilevile hadi ilipokaa sawa.
Saa
mbili baadae ndege ilitua katika uwanja wa ndege wa Zambia na abiria wote
tukashuka na kuelekea hotelini pale
tulikuwa tunatakiwa kesho kushinda kutwa nzima na kuondoka kesho yake.
Tulipata
hoteli nzuri,tulikula chakula ile roho inapenda na soda na kwenda kulala kwa
ahadi ya kesho kwenda kuzunguka mjini tuone ulivyo.asubuhi tukapata breakfast
ya nguvu na kutoka kuelekea mjini kwa miguu ili tuufaidi mji.
Jiji
la Lusaka ni zuri na liko bize ingawa watu walikuwa wanakatazwa kunywa mchana
na serikali lakini bado wanaume wengi mchana walikuwa wanalewa kwa raha
zao.tulipagawa tulipoona supermarket zilizojaa vyakula vya aina mbali mbali
wakati Bongo kila kitu kwa foleni!
Maduka ya viatu ya bata toka sandal hadi viatu vya ngozi ya kupindua!
Tulizunguka
mjini mpaka jioni tukarudi hotelini kujitayarisha kwa safari ya kesho yake…..
Nini
kitatokea katika safari ya kwenda Angola?
Usikose
kufuatilia sehemu ijayo ya mimi na Angola.