Na mwandishi wetuMuongozaji na mwigizaji mahiri Swahilihood Kulwa Kikumba maarufu kama ‘Dude’ anasema kuwa ili tasnia ya filamu isonge mbele lazima wasanii na wadau wote washikane na kuwa kitu kimoja ili kuleta maslahi ya kweli nchini.
Akiongea na Mwandishi wa Filamucentral hivi karibuni, Dude alisisitiza kuwa nguzo kuu ya kufanikiwa kwa tasnia nzima si kwa msaada au juhudi za mtu mmoja, bali ni kwa Taifa zima, hasa wasanii wote kwa ujumla, na ndio maslahi ya kweli yataoneka na kusonga mbele na kuijenga tasnia ya filamu.
![]() |
| Dude akisisitiza Jambo fulani katika mahojiano yake na Mwandishi Studioni. |
zaidi ya hapo, aliongezea kuwa sanaa kwa ujumla inahitaji ushirikiano na mshikamano wa kila Mshiriki katika sanaa, ukianzia kwa wasanii wenyewe, wadau, wawekezaji, pia na kwa serikali yetu pendwa, na pale mmoja akiteleza, inakuwa rahisi kwa wengine kumkumbusha na kumuweka sawa, kama ambavyo wenzetu wa India wanavyokuwa pamoja Filamu ya Udta Punjab inaelezea athari za madawa ya kulevya eneo la Punjab ambapo Central Board of Film Certification iliamua zaidi ya vipande 89 vya filamu hiyo vikatwe kutokana na maoni ya viongozi wa Jiji la Punjab kupinga kuoneshwa kwake kwa jinsi vijana wakiathiriwa na Madawa ya kulevya jimboni humo.
Filamu hiyo, (Udta Punjab) imetoka juni 17 mwaka huu, ikiingiza kiasi cha US$ milioni 7.1 zaidi ya bajeti halisi ya filamu hiyo yenye thamani ya Dola za kimarekani Milioni 5.9
Chanzo, Filamucentral
