MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) umeandaa sherehe za
kumkabidhi eneo la kujenga kituo cha michezo mchezaji bora wa Afrika,
Mbwana Samatta katika sherehe zitakazofanyika Juni 4, 2016 kwenye kijiji
cha Wasani Mwanzega Mkuranga.
Mwenyekiti wa
SHIWATA, Cassim Taalib alisema jana Dar es Salaam kuwa maandalizi ya
sherehe hizo itaambatana na ugawaji nyumba 31 kati ya hizo moja kubwa,
tatu ndogo na misingi 27 ya nyumba hivyo kufikisha jumla ya nyumba 150.
Alisema
baba yake Mbwana Mzee Ali Samatta amethibitisha kuwepo kwa mwanae
katika sherehe hizo ambazo naye ametunukiwa kuwa mwanachama wa heshima
wa mtandao huo na kukubali kushirikiana kuhakikisha michezo inakuwa
nchini.
"Baba yake Samatt alisema wakati akiwa
kijana alikuwa mfungaji mzuri kwa timu alizowahi kuchezea miaka ya
sitini kama vile timu ya shele ya Sekondari ya Mzumbe, timu ya mkoa wa
Morogoro, timu ya Polisi na badaye aliwahi kuichezea Simba akiwa na
akina Hamisi Kilomoni" alisema Taalib.
Alisema
sherehe hizo pia zitapambwa na wasani kutoka vikundi mbalimbali vya
ngoma na sarakasi kutoka jijini Dar es Salaam na mkoa wa Pwani..
Alisema
SHIWATA ilimzawadia uanachama wa heshima mchezaji huyio baada ya
kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa Afrika na kutangaza kumpatia eneo la
ekari tano kwa ajili ya kujenga kituo cha wanamichezo.
BABA
Mzazi wa Mchezaji bora wa Soka bara la Afrika, Ali Samatta (katikati)
akiwa na Katibu Mkuu wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) Michael
Kagondela kulia na Mhasibu wa mtandao huo, Asha Salvador baada ya
kumkabidhi kadi ya uanachama na katiba baada ya kikao cha kuthibitisha
mwanae kukubali kupewa ekari tano za kujenga kituo cha wanamichezo,
Mkuranga.
Picha 0398
BABA Mzazi wa
Mchezaji bora wa Soka bara la Afrika, Ali Samatta (katikati) akiwa na
Katibu Mkuu wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) Michael Kagondela
kulia na Mhasibu wa mtandao huo, Asha Salvador baada ya kumkabidhi kadi
ya uanachama na katiba baada ya kikao cha kuthibitisha mwanae kukubali
kupewa ekari tano za kujenga kituo cha wanamichezo, Mkuranga
Picha 403