Ms Lucy Goes To Africa yafana, Muandaaji aangua kilio jukwaani

Lile onesho la tamthilia ya jukwaani iliyokuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu sana na wakazi wa jiji la dar es salaam, leo limefikia tamati kusubiri na kisha kuoneshwa jioni katika kumbi wa Theatre wa Makumusho ya Taifa uliopo Shabban Robert street, Jijini Dar
sherehe hizo ambazo zilianza na Jazz Party iliyochanganyika na Chakula safi cha jioni kiitwacho "Gumbo", ilianza kufana mapema zaidi ya saa tisa kamili kama ilivyoandaliwa na Mmarekani Toussaint Duchess. wageni waalikwa walianza kufika mapema zaidi, ambapo walikaribishwa na Muziki safi wa Jazz ulioburudishwa na Bendi ya live yenye muimbaji bora kabisa kutoka hapahapa Nchini
Baada ya Vinywaji na Chakula kizuri cha kujihudumia mwenyewe maarufu kama Buffet, sherehe rasmi ilianza jioni ya saa kumi na mbili kwa kuanza kwa play hiyo ya kusiismua ikishirikisha waigizaji nguli katika tasnia ya Filamu nchini akiwaemo Yvonne Cherryl (Monalisa) na Susan Lewis (Natasha) na waigizaji wengine mbalimbali kama vile (Raheem) na wengineo

Tamthilia hiyo ya jukwaani yenye kisa cha Mmarekani aliyekuja Afrika kwa bahati Mbaya, imechezwa vyema na Muigizaji Lady Toussaint Duchess ambaye ameicheza vyema nafasi yake akiigiza kama Lucy (starring)

Filamu hiyo, imekuwa ikiwasisimua watazamaji wake muda wote walipokuwa wanaitazama, ambapo waigizaji wametumia pia sanaa ya uimbaji vizuri katika kunogesha na kufikisha ujumbe kwa hadhira yake, ambapo watazamaji wameonekana kuifurahia vilivyo wakifuatisha baadhi ya nyimbo hizo

kwa upande mwingine, hadithi imekuwa na msisimko wake, baada ya msanii wa zamani maarufu na pia mtangazaji wa kipindi cha danga chee, anayejulikana kama shamsa kutuambia kwa vile jinsi alivyostaajabia sanaa ya Tanzania ikichanganyika na Umarekani inavyoweza burudani ya aina yake
"kiukweli nimefurahi sana na kuburudika vya kutosha kuona namna nguvu ya sanaa inavyojitosheleza kwa hadithi fupi na yenye maana, ikiwa na vitu vyote muhimu katika sanaa (Fani na Maudhui na kisha kwa mtiririko mzuri na wa kipekee. siwezi kusema kuwa hakuna kama ule, la hasha...ila kiukweli ni burudani ya aina yake ambayo ningejutia mno kuikosa"

Nimejisikia faraja sana kuona sanaa ya Tanzania ikizidi kukua, licha ya changamoto mbalimbali zinazotukabili. si kwamba ukifanya kazi na mmarekani ndio unakuwa umemaliza, hapania ila wageni wanapokuja na nchini kwako kwa ajili ya kazi fulani, basi ujue kuwa hilo ni jambo la heri"aliongezea Monalisa

"kwanza sikuamini kama watanzania wangeweza kujitokeza namna hii, ila ni neema ya pekee kwa watanzania kuuonesha upendo wao wa pekee kwetu kwa ajili ya sanaa. Tunawapenda sana."aliongezea Susan

baada ya igizo hilo, alipoambiwa aseme machache kuhusiana na kazi nzima aliyoifanya; ndipo aliposhinwa kuvumilia na kuanza kuyamwaga machozi yake, huku akishuku makampuni, taasisi na vituo mbalimbali na kuthibitisha kuwa haikuwa kazi rahisi.

Chapisha Maoni

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Mpya zaidi Nzee zaidi