Swahiliwood wapata msiba, HAJI JUMBE aaga Dunia

Tanzia
kwa taarifa zilizotufikia hivi punde, ni kuwa Muigizaji na mwanachama wa chama cha waigizaji, na pia mjumbe wa kamati ya uchumi mipango na fedha
Ndugu  HAJI JUMBE

Amefariki muda huu katika hospital ya mvungi kinondoni B. Ndugu Jumbe amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Tumbo, ambapo alifikishwa hospitalini hapo na mauti kumkuta.

kwa taarifa za awali, kutoka kwa Mwenyekiti wa Sherehe, Maafa na Bonanza, Ndugu Salum Chirwa, amesema kuwa msiba utakuwepo Mwananyamala Komakoma, na mengineyo yatafahamishwa muda utakapowadia baada ya taratibu zote za msingi kufuatwa, ikiwemo taratibu za mazishi.
Marehemu amekuwa na mchango mkubwa katika tasnia ya filamu nchini, na amekuwa akiigiza kwenye tamthilia mbalimbali ikiwemo ya Siri za Familia inayoendelea kuoneshwa kwenye kituo kimoja cha televisheni nchini, cha EATV



Chapisha Maoni

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Mpya zaidi Nzee zaidi