ILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA
.......Sijui mama na baba walikuwa wakiwaza nini ila kwa upande wangu nilijiona kuwa nina bahati mbaya maana kama nilivyosema hapo awali ilikuwa ni miezi michache toka nimetenda kosa kubwa maishani na kosa lenyewe linaweza kunifanya nisiende hii safari tofauti na safari zote wanazokwenda wazazi wangu,......
Endelea na sehemu ya pili ya mimi na angola……
....maana safari hii kama ntafanikiwa kwenda (kitu ambacho bado ni ndoto), itakuwa ni safari yangu ya tatu kusafiri nao. Ndugu zangu wanasema mimi ni mtoto mpendwa wa baba, ingawa sina uhakika na hilo kwa sababu baba mwenyewe hajawahi kulitamka neno hili, ila ukweli ni kwamba mimi ni mtoto wa sita katika familia yetu yenye watoto saba, na baba alikuwa mfanyakazi wa wizara ya mambo ya nchi za nje na mama nesi.
Mwaka 1969 baba alipata uhamisho kwenda nchini ufaransa na mimi na mama tulienda pamoja nae, wakati huo nilikuwa mtoto mdogo tu na nasikia nilikuwa bingwa wa lugha ya kifaransa! Unajua watoto wanajifunza lugha upesi nikawa ndio mkalimani wa mama alipokuwa anakwenda supermarket kununua vitu maana yeye lugha ilimpita pembeni kidogo.
Miaka miwili baadae baba alihamishiwa China kama kawa nami nilikuwemo msafarani ila safari hii walimchukua na dada yangu aitwae Rose ninayemfuata. Nakumbuka siku ya kwanza kuona nzi wakianguka toka mbinguni nikamwonyesha Rose ambae nae alishangaa nikaona ni vema kumwita mama nae ajionee maajabu ya china nzi wanaanguka toka mbinguni tena weupe sio kama wale wa bongo.
Mama alikuja balcony tulipokuwepo nae alishuhudia nzi weupe ingawa yeye hakushangaa ila alicheka sana..“sio nzi hawa, hii ni snow (barafu) , ...mkisikia theluji ndio hii”
Tulishangaa! Akatuambia tuweke viganja vyetu kuikinga, tulifanya hivyo na theluji illitua kwenye mkono na baada ya sekunde kadhaa iliyeyuka mbele ya macho yetu. Tulishangaa lakini tulifurahia zoezi hilo na kutufanya tuzidi kulirudia! tuliendelea kubaki palepale kwa muda tukiiangalia theluji ikishuka chini, barabarani na kuifanya barabara igeuke nyeupe.
Eneo tulilokuwa tukiishi lilikuwa la watu wa mataifa tofauti duniani wenye hadhi ya kidiplomat, lilizungushwa ukuta hivyo ukitaka kutoka nje ni lazima upite katika geti na uruhusiwe kuingia au kutoka.
Michezo tuliyoikuwa tukicheza ni kuteleza kwenye theluji au kutengeneza mtu wa barafu tunamwekea pua , mdomo kwa kutumia miti au matawi au matunda yasiyoliwa yanayoanguka toka katika miti inayovumilia wakati wa baridi na mmoja wetu anajitolea kumvalisha kofia yake kisha tunatengeneza matonge ya barafu na kuanza kumpiga nayo mpaka anavunjika vunjika tunafurahia kwa vile eti amekufa!
Tulipewa uamuzi wa kuchagua shule ya kusoma ama ya kichina au shule ya kimataifa inayofundisha kiingereza, mama alituchangulia ya kiingereza ingawa watoto wengine wa familia moja ya kitanzania walikwenda kusoma ya kichina. Sababu kubwa ya mama ilikuwa kiingereza kinazungumzwa dunia nzima lakini kichina ni uchina tu!
International school ilikuwa ikiendeshwa na waasia wenye asili ya Kihindi ilikuwa nzuri ila vitu viwili tu vilinikera kuhusu shule hii, kwanza wakati ya mapumziko tulikuwa tunapewa vitafunio ambavyo mara nyingine huwa ni biskuti na juice au tunda la tofaa (apple) na biskuti hapa ndo nisipopenda tufaa na biskuti? Kwanza sipendi tufaa likikatwa baada ya muda linakuwa na rangi ya hudhurungi pembeni huwa inanichefua kisha tena na biskuti ni sawa na kula ugali na mkate!
Cha pili kilichoniudhi wakati mwalimu wa kike aliekuwa akitufundisha mwandiko kwa kugandamizia inabidi uende mbele kwenye meza ya mwalimu unainama huku ukiandika anakungandamizia na mkono wake sasa tatizo linakuja huo mkono wake ulikuwa unanuka vibaya nilikuwa nakosa raha kila nilipoitwa kwake.
Ila cha kufurahisha China na bado ninakikumbuka ingawa kwa wakati ule nilikuwa bado mdogo ni jinsi wachina walivyokuwa wengi ukitembea barabarani hasa kwenye taa zinaposimamisha magari utaona baiskeli nyingi sana zinangojea taa. (hii naizungumzia china ya miaka ya 70) ukitembea barabarani wachina wanatushangaa utakuta wanaongea kikwao kisha mmoja anajitoa mhanga na kuja kukusugua mkono ilia one kama ni rangi au ni uchafu hatuogagi, wanaporidhika kuwa ni rangi yetu wanaondoka huku wakiendelea kuongea kikwao, hatukuwahi kuwa na marafiki wa kichina ila kwa vile tulikuwa tukikaa eneo la madiplomat tupu hivyo tulicheza wenyewe kwa wenyewe. Watu wa mataifa mbalimbali wanaofanya kazi katika mabalozi.
Nakumbuka siku moja tulikuwa tunacheza jioni maeneo ya kulaza magari mara tukamwona mfanyakazi wa ndani ambae ni mchina anakuja haraka akiwa amehamanika akatukutanisha watoto wote na kutuamuru twende eneo Fulani mle mle kwenye eneo letu la madiplomat na kutuweka pamoja kama vile kuna vita!
Eneo zima lilikuwa limezizima kwa hofu ya sintofahamu.
Ni nini kilitokea mpaka ikatokea hali ya wasiwasi na sintofahamu?
Usikose sehemu ya tatu ya mimi na angola.