Wanachama 300 SHIWATA wajiunga na PPF

Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib (Kushoto) akikabidhi fomu ya Bima ya Afya kwa Ofisa Uendeshaji wa PPF, Tumgonze Kabigumila baada ya kuijaza kwa ufasaha
Na Mwandishi Wetu
WANACHAMA zaidi ya 300 wa Mtandao wa Wasanii Tanzania wamejiunga na Mpango wa Taifa wa Akiba ya Uzeeni (PPF) katika mpango maalum wa Wote Scheme utakaofanya wajiunge na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na kupata mikopo mbalimbali.

Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib alisema jana jijini Dar es Salaam wakati wa kuandikisha wanachama hao kujiunga na PPF na kujaza fomu za Bima ya Afya, alisema kupitia mpango wa "Wote Scheme" wanatarajia kuwashawishi wanachama wao zaidi ya 8,000 kujiunga na mpango huo.
Ofisa wa MAsoko wa PPF, Abib Kibiki (aliyesimama) akiwaelekeza wasanii wa SHIWATA kujaza fomu za kujiunga na PPF na nyingine kujiunga na Bima ya Afya
"Tumepokea kwa furaha mpango wa PPF kutunganisha kupata bima ya Afya, tunatarajia wanachama wettu wote wajiunge ili wapate huduma muhimu za matibabu na mikopo mbalimbali kwa maendeleo yao na familia zao" alisema Taalib.
kwa upande wake, Afisa Uendeshaji wa PPF, Tumgonze Kabigumila alisema PPF imejizatiti kusaidia jamii ya watanzania kupata huduma muhimu za kijamiii kwa gharama nafuu.
Alisema katika mpango huo unajikita zaidi katika kuwasaidia watanzania wasio katika sekta rasmi kama vile wavuvi, wakulima, wajasiriamali, wanamichezo na wasanii kupata huduma muhimu na za msingi.
Aliongezea kwa kusema kuwa kiasi cha chini cha mwanachama kuchangia kwa mwezi ni Tshs. 20,000/= tuu kila mwezi na ataanza kupata matibabu akikamilisha Tshs. 60,000/=  tu ambapo atapewa kadi ya bima ya afya ambayo ataitumia katika hospitali zote nchini kwa matibabu yake mwenyewe (mhusika) ya magonjwa mbalimbali.
Katibu Mkuu wa SHIWATA, Michael Kagondela (kulia) akisaidiana na wasanii wa SHIWATA kujaza fomu za kujiunga na BIMA ya Afya zinazosimamiwa na PPF
Tags: SHIWATA, PPF

Monalisa Tanzania

Hi! karibu katika blogsite yangu ya Monalisatanzania. upate kunifahamu japo kwa ufupi na kipekee kama shabiki au mpenzi wa kazi zangu. utapata habari, burudani na taarifa official kutoka kwangu. enjoy!

Chapisha Maoni

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Mpya zaidi Nzee zaidi