| M/kiti wa TDFAA, Ally Baucha (kulia) na katibu wake, Jafari Makatu (kushoto), wakiwa katika kikao cha TDFAA kilichofanyika Jumamosi |
Akizungumzia kuhusu uteuzi huo, mara baada ya kutangaza kamati hizo, Katibu wa chama hicho ndugu Jafari Makatu (maarufu kama mzee chumo) amesisitiza kuwa wanachama hao waliochaguliwa wanapaswa kufanya kazi kwa bidii, bila ya kujali manenomaneno ya pembeni kutoka kwa watu wasio na uhalali na chama hicho
“Sifa ya mwanachama bora wa kikundi chetu ni kuwa hai. Hivyo, viongozi hawa tuliowachagua leo kama kikundi wamapaswa kufanya kazi kwa bidii pasipo kujali maneno wala ushauri wa pembeni, hasa kutoka kwa mtu asiyehusika na Chama chetu.”
Kwa upande wake, mwenyekiti wa chama hicho (TDFAA) Ally Mohamed Baucha amefurahia kikao hicho na kudai kuwa kimejadili vizuri maridhiano ya migogoro ya muda mrefu baina ya wanachama wa vikundi vingine mbalimbali na utambulisho wa Vyama maalum vinavyotambuliwa na Shirikisho la Filamu Nchini (TAFF)
| Mmoja wa wajume wa kikao hicho akitoa maoni yake kwenye baadhi ya ajenda za kikao hicho |
Kamati zilizoundwa kwenye kikao hicho pamoja na kamati ya Uchumi mipango na Fedha, kamati ya Pili ni Sherehe na Maafa, kamati ya Tatu ni Elimu na Mafunzo, Kamati ya nne ni Baraza la Wazee na Kamati ya Tano ni Nidhamu na Maadili.
“Ni vyema wanachama wetu wawe hai, kwa maana sisi tunasisitiza sana Umoja. Mwisho wa wanachama wafu ni wiki ijayo. Wanapaswa wahakikishe wanafuata taratibu zote za kuwa mwanachama hai wa TDFAA. Kwa wanachama wapya, taratibu zetu za kujiunga ni rahisi zaidi, uwe na miaka 18 au zaidi, uwe unacheza Filamu na/au kikundi cha sanaa na unachukua fomu ya kikundi chetu na kuijaza ikiwa na passport size mbili.” Aliongezea Ally Baucha
| Mgeni wa kikao hicho, Obugwai Izoba akitoa neno |
“Ninaamini kabisa wasanii ninaoongea nao wanan nia ya dhati kwa maendeleo ya sanaa nchini.”
Mgeni huyo, anayefahamika kwa jina la Obugwai izoba awashauri pia wasanii kufikiria soko la nje ya chini, akidai kuwa soko linasubiria wasanii wa Tanzania, na si vinginevyo.
“Naomba tufikirie kutafuta Masoko Nje ya Tanzania kwani watanzania wako Byee, braviee, tena braviee ya nguvu.tukijitokeza na kuitumia fursa hiyo ya Nje ya Tanzania, tutaweza kulitawala soko hilo vizuri, hasa nchi za Congo (DRC), Burundi, Rwanda, Uganda na Nchi nyingine jirani”
Kikao hicho kilihudhuriwa na wanachama hao wa TDFAA wakiwemo mastaa mbalimbali kilichofanyika hoteli ya Traverntine Magomeni, Jijini Dar es salaam.
| Mmoja wa Wajumbe (bichani kulia) wa kamati hizo akisisitiza jambo katika kikao hicho. kikao hicho kilifikia muafaka wa malengo mbalimbali |