Na Mwandishi wetu
Shirikisho la Filamu Nchini (TAFF) limekaribisha wadau wote wa filamu nchini kushiriki katika StreamEast, jukwaa jipya la kidijitali linalowezesha uuzaji na usambazaji wa kazi za filamu.
Akizungumza kwa niaba ya shirikisho hilo, Ndugu Maja Matata alisema kuwa StreamEast linajumuisha kazi mbalimbali za filamu kutoka mashirikisho ya filamu zaidi ya saba barani Afrika.
"Nchi wanachama wanapata fursa ya kuwahamasisha wanachama wao kuwasilisha kazi zao kwa utaratibu rahisi na wezeshi, ili ziweze kuoneshwa kwenye jukwaa hili linalofikisha kazi za filamu kusini mwa Jangwa la Sahara. Kila siku tunapokea kazi mpya, na faida yake si kwa producer pekee, bali pia kwa mtunzi na kikosi kizima kilichoshiriki," alisema Bw. Matata.
Kwa sasa, nchi wanachama wa jukwaa hilo ni Kenya, Uganda, Tanzania, Ethiopia, Angola, Zambia, Rwanda na Burundi, huku likitarajiwa pia kuhusisha nchi za kusini mwa Afrika zikiwemo Afrika Kusini na zingine mbili.
StreamEast itahusisha aina zote za kazi za filamu ikiwemo makala, filamu fupi, filamu ndefu na tamthilia.