Kicheche Mr Makoti kuwania Tuzo za Iconic Awards 2025


Uploading: 200853 of 200853 bytes uploaded.

Na Mwandishi wetu

Msanii wa maigizo anayetikisa mitandaoni, Kicheche Mr Makoti, ameendelea kuipeperusha bendera ya Tanzania baada ya kuteuliwa kuwania tuzo za Iconic Awards Uganda kwenye kipengele cha Best Comedian – Comedy Category.

Katika tuzo hizo za kimataifa, Mr Makoti ameingia kwenye orodha ya wasanii watakaopigiwa kura na mashabiki kutoka pembe zote za dunia kupitia tovuti rasmi ya tuzo hizo, hatua inayompa nafasi ya kipekee kuonesha ubora wa vipaji vya waigizaji wa vichekesho kutoka Tanzania.

Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, msanii huyo alionyesha kufurahishwa na hatua hiyo, huku akiwashukuru na kuwaomba mashabiki wake kuendeleza sapoti.

“Wana Familia, Hii tuzo ni ya kwetu… Nawategemea sana.” aliandika kwenye chapisho lake la instagram

Uteuzi wake umeibua gumzo mtandaoni, na mashabiki pamoja na wadau wa tasnia ya filamu wameanza kampeni za kuhamasishana kumpigia kura ili kumwezesha kushinda tuzo hiyo kubwa.

Tuzo za Iconic Awards kwa mwaka huu zimeweka kipengele kimoja tu kwa waigizaji, huku maeneo mengine yakitawaliwa na wasanii wa muziki na mitindo. Hii imefanya nafasi ya Mr Makoti kuwa ya kipekee na yenye ushindani mkubwa.

Kwa mujibu wa taarifa za waandaaji wa tuzo hizo, hafla ya utoaji wa tuzo inatarajiwa kufanyika Desemba 20, 2025 jijini Kampala, Uganda, ambapo wasanii kutoka mataifa mbalimbali watahudhuria katika usiku wa kutunza vipaji vya Afrika Mashariki

Chapisha Maoni

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Mpya zaidi Nzee zaidi