Na Mwandishi Wetu
Chama cha Waigizaji Tanzania (TDFAA) kimemteua Ndugu Salum Chilwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa chama hicho, kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Ndugu Silvanus Mumba.
Uteuzi huo umefanywa na Mwenyekiti wa TDFAA Taifa, Bw. Chiki Mchoma, na umetangazwa rasmi leo, Januari 12, 2026.
Ndugu Chilwa anachukua wadhifa huo baada ya Ndugu Silvanus Mumba kuamua kuachia nafasi yake kutokana na kubanwa na majukumu mengine ya kikazi.
Uongozi wa chama umeeleza kuwa uamuzi wa Mumba umefanyika kwa heshima na kwa maslahi mapana ya chama.
Akizungumzia mabadiliko hayo, uongozi wa TDFAA umeeleza kuwa Katibu Mkuu mpya ataleta nguvu mpya katika kuimarisha sekta ya filamu na sanaa ya uigizaji nchini, hususan katika kusimamia maslahi ya wasanii na kuimarisha mifumo ya chama.
Chama kimewataka viongozi na wanachama wote kumpa ushirikiano wa karibu Katibu Mkuu mpya ili kuhakikisha mafanikio yaliyopatikana yanaendelezwa na changamoto zilizopo zinapatiwa ufumbuzi.
TDFAA inatarajia kufanya chaguzi zake mbalimbali kuanzia ngazi ya wilaya hadi taifa ndani ya mwaka huu, kwa kuzingatia maelekezo ya wizara husika, hatua inayolenga kuimarisha uwazi, uwajibikaji na demokrasia ndani ya chama