Isarito: “Hadithi za Kitanzania sasa zinaanza kuonekana duniani”


Na Mwandishi wetu

Muigizaji na mtayarishaji wa filamu Isarito ameendelea kusherehekea mafanikio ya My Son baada ya filamu hiyo kuendelea kupata recognition katika majukwaa mbalimbali ya kimataifa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Isarito aliandika ujumbe uliobeba hisia na tafakari kuhusu safari ya filamu hiyo, akisema, “Giza lilikuwa darasa kwetu My Son na mwanga ni matokeo.”

Muigizaji huyo pia aliishukuru Africa Magic kwa kuitambua “My Son” kupitia jukwaa la AMVCA 2026, huku akieleza kuwa hatua hiyo ni ishara kwamba hadithi za Kitanzania zinaanza kupata nafasi kubwa zaidi kwenye soko la kimataifa.

“KWA muda mrefu tumekuwa watazamaji wa hadithi kutoka kwingine. Sasa dunia inaanza kutazama hadithi zetu,” aliandika Isarito.

“My Son” imeendelea kuwa moja ya filamu zilizotikisa mwaka huu baada ya kushinda tuzo sita kwenye TAFFA Awards, huku pia ikifanikiwa kushinda kipengele cha trailer kwenye Filmmakers Hangout nchini Kenya.


Mbali na ushindi huo, filamu hiyo pia imepata nafasi katika majukwaa na tamasha mbalimbali ikiwemo ZIFF Awards, Filmmakers Session Vol. 3 nchini Marekani, Egyptian American Film Festival nchini Misri pamoja na Entertainment Week Africa nchini Afrika Kusini.

Kwa mujibu wa Isarito, mafanikio hayo si ya bahati bali ni matokeo ya kazi, uthubutu na imani kwamba simulizi za Kitanzania zina uwezo wa kushindana kwenye kiwango cha dunia.

“Hii ni uthibitisho kwamba hadithi za Kitanzania zinaweza kusimama, kushindana na kushinda kimataifa,” ameongeza.

Katika kipindi cha karibuni, “My Son” imeendelea kupata attention kubwa kutoka kwa wadau wa filamu ndani na nje ya Tanzania, huku wengi wakiiangalia kama moja ya kazi zilizofungua njia mpya kwa sinema ya Tanzania kwenye soko la Afrika na dunia kwa ujumla.



Chapisha Maoni

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Mpya zaidi Nzee zaidi