By Charles Mkoka
Documentary (Makala) inayozungumziwa sana kwenye eneo la utalii na mazingira, Guardians of the Peak, leo inatarajiwa kuoneshwa rasmi jijini Dar es Salaam kupitia screening maalum itakayowakutanisha wanafunzi wa vyuo, wadau wa filamu pamoja na vijana wenye interest na utalii, mazingira na storytelling.
Screening hiyo itafanyika EACLC kuanzia saa 10 jioni hadi saa 12 jioni, ikiwa sehemu ya kampeni ya kuhamasisha kizazi kipya kuhusu umuhimu wa uhifadhi wa mazingira na kuitangaza Tanzania kupitia filamu.
“Guardians of the Peak” ni documentary inayochunguza safari ya Mlima Kilimanjaro huku ikigusa masuala ya utalii endelevu, mabadiliko ya tabia nchi, utunzaji wa mazingira pamoja na ushirikiano wa kitamaduni. Filamu hiyo imeongozwa na Ram Ally kwa kushirikiana na Elizabeth Mrembo.
Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali za mradi huo, documentary hiyo imekuwa sehemu ya juhudi za kuitangaza Tanzania kimataifa kupitia simulizi zinazogusa mazingira na utalii, huku Mlima Kilimanjaro ukiwekwa kama alama kuu ya kampeni hiyo.
Mbali na screening, tukio hilo litakuwa na mijadala kuhusu mazingira, utalii, pamoja na experience sharing kutoka kwa wanafunzi wa vyuo vikuu waliohusika au kuvutiwa na project hiyo.
Waandaaji wanasema lengo si kuonyesha makala pekee, bali kuanzisha mazungumzo mapya kuhusu namna vijana wanavyoweza kutumia filamu na maudhui ya kidigitali kuhamasisha uhifadhi wa mazingira na kuitangaza Tanzania duniani.
Tangu kuzinduliwa kwake mwaka jana, “Guardians of the Peak” imeendelea kupata hamasa kubwa kutoka kwa taasisi za utalii, mazingira na filamu kutokana na ujumbe wake kuhusu uhifadhi wa Mlima Kilimanjaro pamoja na matumizi ya filamu kama nyenzo ya kuhamasisha mabadiliko ya kijamii.