Tuzo za filamu nchini
zinaendelea kupamba moto kwa hatua mbalimbali kukamilika kwa mafanikio makubwa.
kwa zoezi la uwasilishaji
tuzo, linatarajia kufikia tamati Tarehe 31 ya mwezi huu, ili kupisha mchujo
wake.
akitoa maoni yake kuhusiana
na tuzo hizo, mwenyekiti wa TDFAA Iringa, Ndugu Khamis Nurdin Amesema kuwa Uwasilishaji
na Upokeaji wa Tuzo za Filamu Nchini ni hatua muhimu katika kukuza na
kuendeleza tasnia ya filamu nchini.
“Chini ya usimamizi wa Bodi
ya Filamu, mchakato huu huimarisha heshima na hadhi ya wasanii, huku ukitambua
ubunifu, ubora na mchango wao katika sekta ya burudani.” alisema Nurdini
Mwka huu, mchakato rasmi wa
usaili unahusisha matumizi ya teknolojia mabapo mshiriki anatuma kazi yake
mtandaoni (Online) kwa mfumo maalum wa tovuti kwa anuani ya www.taffafestival.or.tz/tuzo ili
kujisajili na kuwasilisha filamu zao
“Mfumo wa kitaalamu wa
uteuzi, upimaji na utoaji wa tuzo unahakikisha uwazi, usawa, na uhalali wa
matokeo.”
akifafanua kuhusiana na
fursa za kimaendeleo, Amesema kuwa tuzo hizo ni ishara ya ukuaji wa sekta ya
filamu Nchini kwani fursa zinajionesha wazi, hata kama hazijashikiwa mabango
“kuwa na Tuzo imara kunachochea
ushindani wa kimaendeleo, kuvutia wawekezaji, na kuongeza hamasa kwa wasanii
chipukizi. Kwa ujumla, Bodi ya Filamu inapoweka taratibu na vigezo vya uwazi,
hujenga imani kwa wadau na kuimarisha nafasi ya filamu za Tanzania katika soko
la kitaifa na kimataifa.” aliongezea MwenyekitI huyo
Tangu kuanza kwake mwaka
2021, mwamko umekuwa ukiongezeka katika kila tamasha, na kualika wataalamu wengi
zaidi wa kitaifa na kimataifa