Rais wa TAFF Atembelea Kituo cha KBS Korea

Na Mwandishi wetu

Seoul. Rais wa Shirikisho la Filamu Nchini (TAFF), Rajabu Amiry, ametembelea kituo cha kurusha matangazo ya televisheni, redio na makala cha Korean Broadcasting System (KBS) jijini Seoul, Korea Kusini.

Matembezi hayo yamefanyika wiki hii akiwa pamoja na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Nchini (TFB) Dkt. Gervas Kasiga, pamoja na watumishi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na wadau wa sekta ya filamu.

matembezi hayo yamelenga kujifunza zaidi kuhusu uendeshaji na urushaji wa matangazo katika kituo hicho, chachu inayokusudiwa kuhamasisha maendeleo ya sekta nzima ya filamu nchini.

Wakiwa Korea, timu nzima kutoka nchini Tanzania ilitembelea Korea Film Archive (KOFA) pamoja na maeneo mengine muhimu, ikiwemo mafunzo ya utunzaji wa mazingira ya baharini yanayohusiana na vivutio vya utalii.

Ujumbe huo ulihudhuria maandalizi yanayoendelea ya Tamasha la kimataifa la filamu la Busan maarufu kama (BIFF) linalotarajiwa kuanza Septemba 20 mwaka huu.

“Ziara hii ilianzia kwenye ratiba ya kimasomo katika mji wa Busan, katika Chuo Kikuu cha DSU, chuo kinachojulikana duniani kwa kutoa elimu ya filamu,” alisema Bw. Amiry.

Chapisha Maoni

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Mpya zaidi Nzee zaidi