Chama cha Waandaaji wa Filamu Nchini (TAFIDA) kimefungua rasmi usaili maalum kwa watengeneza filamu wote nchini, lengo likiwa ni kuhakikisha kila mwongozaji na muandaaji anapata nafasi ya kushiriki katika kujenga mustakabali wa tasnia.
Kwa mujibu wa Katibu wa chama hicho, waandaaji wanahimizwa kujaza fomu ya usaili, iwe ni kwa wale ambao tayari ni wanachama au hata kwa wale ambao bado hawajajiunga.
Hatua hiyo inalenga kukusanya nguvu ya pamoja ili kuandaa mikakati madhubuti ya maendeleo ya tasnia ya filamu bila kurudi nyuma.
“Tunataka kila mwongozaji apate huduma stahiki na fursa sawa, sambamba na kuandaa mkakati wa pamoja wa kulisukuma gurudumu la filamu mbele. Hii ni nafasi ya kipekee kwa wote walio tayari kwa maendeleo,” alisema Katibu wa chama hicho.
Waandaaji wa filamu wanahimizwa kujaza fomu kupitia kiungo hiki
Chama kimeahidi kwamba kupitia zoezi hilo, kitawaunganisha wadau wote kwa pamoja na kuweka misingi thabiti ya kukuza sekta ya filamu nchini.