TDFAA Mkoa wa Iringa Yaandaa Msimu wa Tatu wa Iringa Awards

Na Mwandishi wetu

Iringa – Chama cha Waigizaji nchini (TDFAA) Mkoa wa Iringa imeanza maandalizi ya msimu wa tatu wa Tuzo za Filamu za Mkoa wa Iringa (Iringa Awards), tukio linalolenga kuhimiza ubunifu na kusherehekea vipaji vya filamu mkoani humo.

Akizungumza kuhusu tuzo hizo, Mwenyekiti wa TDFAA Mkoa wa Iringa, Bw. Khamis Nurdin, amesema kuwa tuzo hizo zinabeba taswira ya kipekee, zikishirikisha wadau wengi zaidi na kuhamasisha zaidi kuliko inavyotarajiwa.

"Tunashukuru kuwa tunapata mwamko mzuri kutoka kwa wasanii na wadau mbalimbali, huku wengine wakionesha nia ya kutusapoti," alisisitiza Bw. Khamis Nurdin

Tuzo hizo zinatarajiwa kufanyika tarehe 28 Novemba mwaka huu katika ukumbi wa Royal Palm, Gangironga, Iringa. 

Bw. Nurdin amebainisha kuwa, kutokana na ongezeko la filamu nzuri zilizotengenezwa, mwaka huu mashindano yanadhaniwa kufana zaidi.

"Watu wanapenda filamu zetu na mwaka huu tunatarajia ushindani mkali kwani tuna filamu nyingi nzuri na za kuvutia" aliongeza.

Tuzo za mwaka huu zinaendana na kaulimbiu ya kuunga mkono uwekezaji katika sanaa, ili kuleta maendeleo chanya na ya haraka kwa wanatasnia na kukuza utalii.

Tuzo hizo zinashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo kampuni ya Miale Film Production katika maandalizi na utekelezaji wake.

Chapisha Maoni

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Mpya zaidi Nzee zaidi