Checkbudi afunguka: “Sina nyumba, sina gari... Maisha ni mtihani!”

Na Mwandishi wetu

Msanii wa maigizo anayefahamika kwa jina la Checkbudi ameweka wazi upande wa pili wa maisha yake, akisema kwa sasa anapitia changamoto ngumu licha ya umaarufu alionao kwenye tasnia ya filamu.

Katika mahojiano yanayotrendi mtandaoni kupitia kipindi cha Refresh kinachorushwa na Wasafi TV, Checkbudi alionekana mwenye utulivu lakini akifunguka undani wa hali yake ya maisha.

“Maisha yana mitihani yake. Sina nyumba wala gari mjini hapa. Naishi kwa kuungaunga tu. Ukipenda kunipakazia, fresh tu, nipakazie,” alisema kwa sauti ya utani lakini iliyojaa hisia tofauti ndani yake.

Msanii Mohamed Nurdin, Checkbudi aliongezaea kuwa changamoto hizo hazikuanza jana  kwani amekuwa akipambana tangu kabla hajawa staa, na hata baada ya kujulikana, maisha bado yamempa mafunzo mbalimbali.

“Nilikuwa na gari zamani, lakini ilipata mitihani. Kwa sasa natumia usafiri wowote, bodaboda, daladala, chochote kinachopatikana. Muhimu maisha yanasonga mbele. Ukiona mchongo, nipe basi, nisidhalilike mjini,” alisema kwa tabasamu.

Kauli hiyo imezua mjadala tofauti mtandaoni, huku wengine wakimuonea huruma, wengine wakiamini ni utani wake wa kawaida tuu wa hapa na pale.

Mmoja wa mashabiki aliandika kwenye instagram, "Unajua Checkbudi ni msanii wa vituko, usikute anatuchora tu kama kawaida yake.”

Mwingine akaongeza kwa utani: “Huyo ni mtoto wa Ilala bana, ogopa mtu anayeongea huku anacheka namna ile!”

Licha ya maoni tofauti, wapo waliopongeza ujasiri wake wa kusema ukweli kuhusu hali halisi ya maisha, jambo ambalo mastaa wengi nchini wanalifumbia macho, huku mara nyingi huonekana wakiishi maisha ya kifahari.

Mahojiano hayo yalichochewa kwa swali kuhusu lini mara ya mwisho alikutana na Diamond Platnumz, swali ambalo lilimrudisha mbali zaidi..

Chapisha Maoni

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Mpya zaidi Nzee zaidi