Bodi ya Filamu Tanzania yawahimiza wanatasnia kujirasmisha ili kupata fursa za kitaifa na kimataifa


Na Mwandishi wetu 

Dar es Salaam — Bodi ya Filamu Tanzania (TFB) imewakumbusha wanatasnia wa filamu na michezo ya kuigiza nchini umuhimu wa kujirasmisha na kutambuliwa rasmi, 

Kwa mujibu wa Bodi hiyo, kumekuwa na ongezeko kubwa la fursa mbalimbali zinazotokana na jitihada za TFB kupitia mashirikiano na wadau wa filamu na sanaa za maonesho ndani na nje ya nchi. 

Hata hivyo, wanatasnia ambao hawajajiandikisha rasmi wanakosa fursa hizo kutokana na kukosa utambulisho wa kisheria.

TFB imewahimiza wanatasnia wote ambao bado hawajasajiliwa kuchukua hatua mara moja ili wasiachwe nyuma, huku ikitoa wito kwa wanatasnia waliosajiliwa kuwashirikisha wenzao na kuwahamasisha kufanya usajili.

Baadhi ya fursa zinazopatikana kupitia usajili wa Bodi ya Filamu Tanzania ni pamoja na kushiriki matamasha rasmi ya filamu, mafunzo ya kitaaluma ndani na nje ya nchi, ziara rasmi za serikali na wanatasnia, pamoja na fursa za kushiriki utayarishaji wa filamu za kimataifa (co-productions).

Fursa nyingine ni pamoja na mialiko ya kimataifa ya filamu, safari za kikazi nje ya nchi, na ushiriki katika miradi mbalimbali ya filamu kwa kushirikiana na wadau wa kimataifa.

Bodi ya Filamu Tanzania imeeleza kuwa usajili unafanyika kupitia mfumo wa AMIS, ambapo wanatasnia wanaweza kujisajili kwa kufika katika ofisi za TFB au kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo www.sanaa.go.tz

.

Chapisha Maoni

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Mpya zaidi Nzee zaidi