Na Mwandishi wetu
Watayarishaji na waongozaji wa filamu fupi nchini Tanzania wametakiwa kuwasilisha kazi zao ili kushiriki katika NGALABI SHORTS, jukwaa linalolenga kukuza ubunifu, sauti mpya na hadithi za Kitanzania kupitia filamu fupi.
Kwa mujibu wa waandaaji, mashindano hayo yako wazi kwa watayarishaji wenye umri wa miaka 18 na kuendelea, huku waombaji wakitakiwa kuwa na haki zote za kisheria za uoneshwaji wa filamu zao.
Waombaji wanapaswa kuwasilisha synopsis ya filamu yenye maneno kati ya 100 hadi 150, pamoja na wasifu wa Mwongozaji (Director) wenye urefu wa maneno 100 hadi 150, unaoeleza historia yake ya kazi na mtazamo wa kisanaa.
Aidha, waombaji wanatakiwa kutuma picha tatu za mwongozaji wa filamu zenye ubora wa juu (300 dpi), pamoja na picha tatu za filamu (screengrabs) zenye viwango hivyo hivyo vya ubora.
Kwa upande wa vigezo vya kazi, filamu inayowasilishwa haipaswi kuzidi dakika 30, na lazima iwe na subtitles za lugha ya Kiingereza ili kuwezesha uelewa kwa hadhira pana ya kimataifa.
Maombi yote yanapaswa kutumwa kupitia barua pepe hii: curator.ngalabishorts@gmail.com
NGALABI SHORTS inapokea filamu fupi pekee, na mwisho wa kuwasilisha maombi ni tarehe 28 Februari 2026.
Watayarishaji wanahimizwa kutembelea ukurasa wa instagram wa @ngalabishorts kwa taarifa zaidi, pamoja na kushirikisha wana tasnia wengine wa filamu kwa kushare ujumbe huu ili kuongeza uwakilishi wa filamu za Kitanzania