Sinema Connect North kuwakusanya watengeneza Filamu 2026


Na Mwandishi wetu

Mpango huo unaofanyika kwa mara nyingine tena, unalenga kuwahusisha vijana waliopo katika mchakato wa utengenezaji filamu, wakiwemo waongozaji, waandishi wa miswada, wapiga picha wa filamu (DOPs), wahariri, wataalamu wa sauti pamoja na wasimuliaji wenye maono mapana ya kisanaa na kijamii.

Kupitia Sinema Connect North, washiriki watapata fursa ya kushiriki katika safari ya ubunifu inayochochea mijadala ya kweli ndani ya jamii, huku filamu zikitumika kama chombo cha kuleta mabadiliko chanya na kujenga mshikamano wa kijamii.

Mpango huo unatekelezwa kwa msaada wa VIJANA@rtWORK, ambao unalenga kuwawezesha vijana wabunifu kutumia sanaa na maudhui ya kidijitali katika kuimarisha umoja na mshikamano wa jamii nchini.

VIJANA@rtWORK: Creative Youth for Social Cohesion Across Tanzania inawezeshwa na Goethe-Institute Tanzania kwa kushirikiana na Culture and Development East Africa (CDEA), kwa ufadhili wa Umoja wa Ulaya (EU).

Sinema Connect North ni mradi unaotekelezwa katika mikoa ya Arusha na Manyara ukiwa na lengo kuu moja, kuimarisha uelewa wa jamii juu ya athari zisizo na uwiano za mabadiliko ya hali ya hewa kwa maisha ya watu wa kiasili, huku ukiwawezesha vijana kutoka jumuiya hizi kubuni na kuendesha suluhu zao wenyewe.

Washiriki wanaochaguliwa ni 10, kipaumbele kitapatiwa kwa watengenezaji filamu kutoka katika jumuiya za kiasili kutoka mikoa ya Arusha na Manyara, kutuma maombi na hasa kujaza fomu kwa link ifuatayo: Jisajili Call for Filmmakers

Tarehe ya mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 27 Februari mwaka huu.

Sinema Connect North inatekelezwa na kusimamiwa na shirika la MEDEA Tanzania kwa kushirikiana na YouthHub Arusha (MSTCDC) kupitia ufadhili wa mradi wa VIJANA@rtWORK: Vijana Wabunifu kwa Mshikamano wa Kijamii Tanzania chini ya udhamini na uangalizi wa  Goethe-Institute Tanzania kwa kushirikiana na Culture and Development East Africa (CDEA), kwa ufadhili wa Umoja wa Ulaya (EU)

Watengenezaji wa filamu wenye nia ya kushiriki wanahimizwa kutembelea kurasa rasmi za waandaaji kwa maelezo zaidi na taratibu za kuwasilisha maombi yao.

Chapisha Maoni

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Mpya zaidi Nzee zaidi