Na Mwandishi wetu
Kuna kipindi si cha mbali sana ambapo mafanikio ya filamu Tanzania yalikuwa yanapimwa kwa vitu viwili tu — DVD zimesambaa kiasi gani, au movie imewekwa kwenye flash za Kariakoo mara ngapi.
Ukiona filamu yako inauzwa kwenye mabasi ya mikoani, basi tayari ulikuwa “umefika”.
Leo hii dunia imebadilika.
Audience wa sasa hawasubiri tena CD. Hawataki kusikia “nitakutumia kwa Bluetooth.” Watu wanataka kufungua simu, kubonyeza app, na ndani ya sekunde chache waanze kuangalia kitu chenye quality nzuri. Ndiyo maana streaming platforms zimeanza kubadilisha kila kitu kuhusu namna filamu za Tanzania zinatengenezwa, zinavyouzwa, na hata namna zinavyotazamwa.
Na kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu, industry inaanza kulazimika kufikiria beyond mipaka ya Tanzania.
Miaka michache iliyopita, producers wengi walikuwa wanatengeneza filamu kwa kufikiria soko la ndani pekee. Lakini leo ukijua project yako inaweza kuonekana Kenya, Ghana, South Africa au hata Marekani kupitia streaming platform, ghafla standards zinaanza kupanda.
Kwa sababu audience wa Netflix hawezi kukusamehe kwa audio mbovu.
Hapo ndipo pressure mpya imeingia kwenye industry.
Streaming imebadilisha si tu distribution, bali hata psychology ya utengenezaji wa filamu. Producers wanaanza kuelewa kwamba audience wa sasa wana options nyingi sana. Ndani ya dakika moja mtu anaweza kutoka kuangalia series ya Korea, akaenda Hollywood, akarudi Nollywood, halafu akakutana na filamu yako ya Kiswahili. Ushindani umehamia moja kwa moja kwenye screen moja.
Na ukweli ni kwamba hiyo imeanza kuifanya industry ya Tanzania ijitazame upya.
Kwa muda mrefu tulizoea kutengeneza filamu kwa haraka sana. Wakati mwingine script ikiandikwa Jumatatu, shooting inaanza Alhamisi. Na somehow watu walikuwa wanaendelea kuangalia. Lakini streaming imekuja na audience mpya ambao wanaangalia details. Wanaona colour grading, wanaisikiliza sound design, wanaangalia acting, pacing ya scenes na hata continuity errors.
Sasa hivi ukikosea glass mezani kwenye scene, kuna mtu Twitter atagundua ndani ya dakika tatu.
Lakini pamoja na pressure hiyo yote, streaming platforms zimeleta opportunity kubwa kuliko ambavyo industry nyingi za Afrika zilikuwa nazo zamani.
Kwa mara ya kwanza, filmmaker mdogo kutoka Mbeya, Mwanza au Kigoma anaweza kutengeneza kazi nzuri na ikafika audience ya kimataifa bila kupitia mfumo wa zamani wa distributors wakubwa. Hilo peke yake limebadilisha mchezo.
Na tayari dalili zinaonekana.
Kizazi kipya cha filmmakers kinaanza kuelewa visual storytelling kwa kiwango tofauti. Wengine wanaangalia cinema ya dunia, wanajifunza editing styles mpya, wanajaribu cinematic lighting, na wanaanza kutengeneza filamu ambazo zinaonekana less “video” na more “cinema.”
Hata waigizaji wameanza kubadilika.
Streaming platforms zimeua kidogo ule uigizaji wa “kupaza sauti kila scene.” Audience wa leo wanataka realism. Wanataka performances ambazo zinaonekana kama maisha halisi, si kama watu wanagombania urithi kwenye loudspeaker.
Lakini pamoja na mabadiliko hayo yote, bado kuna changamoto kubwa.
Tatizo kubwa si talent. Tanzania ina storytellers wengi sana. Changamoto ni consistency, uwekezaji na understanding ya biashara yenyewe. Baadhi ya producers bado wanaiona streaming kama sehemu ya “kuweka tu movie” badala ya ecosystem nzima inayohitaji strategy, branding na ubora wa muda mrefu.
Kwa sababu ukweli ni huu — streaming platforms hazibadilishi industry automatically.
Zinaongeza ushindani.
Na kwenye ushindani huo, wale watakao survive si lazima wawe wanaotoa filamu nyingi zaidi. Mara nyingi watakuwa wale wanaoelewa audience wa kisasa wanataka nini.
Huenda hicho ndicho kipindi ambacho tasnia ya filamu Tanzania imekuwa ikikisubiri kwa muda mrefu.
Kwa sababu kwa mara ya kwanza, dunia nzima ipo mfukoni mwa audience… na pia ipo mfukoni mwa filmmaker mwenye idea nzuri.